Nisichopenda kabisa jijini DSM

Nisichopenda kabisa jijini DSM

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2009
Posts
2,988
Reaction score
3,545
kati ya vitu ambavyo sivipendi kabisa ktk jiji la Dsm ni
1] Foleni zisizo na sababu
2] Hakuna maji na umeme wa uhakika
3] .....
 
Wingi wa watu, na kila kukicha watu wanazidi kumigrate kuja Dar.
 
Daladala kupark kila mahali wakati wa kupakia na kushusha abiria,omba omba kila sehemu za makutano ya barabara,
 
Wingi wa watu, na kila kukicha watu wanazidi kumigrate kuja Dar.
Mweh...we hupendi watu? as for me, I get my strength from God and aspiration from them people

.....maji machafu na yanayonuka kila mtaa
 
Harufu ya mkojo (kuanzia unaposhuka airport hadi mitaani..)
 
huduma zote muhimu kupatikana eneo moja
 
Nilishapungua huko siku nyingi, usijali sana

BTW asante kwa ushauri.
Noted with appreciation!

2010, VITENDO ZAIDI!..achana na hawa wanaolalamika wee, lakini wamekomalia hukohuko, utasema kwingine ni Falluja!😀😀..

Nchi hii ni pana jamani..kuna sehemu zingine huku hatujui shida ya maji wala foleni, wala joto, wala msongamano,wala adha ya machinga, wala shida ya wapiga debe..

Tunapeta tuu!
 
joto kali hasa kwa watumia daladala, mmebanana na mnavuja majasho, hatari kwa maambukizi ya magonjwa ya ngozi!
 
marundo ya uchafu kila sehemu.......
 
1) Mabango ya biashara kila mahali, mirangi rangi tu isiyokuwa na mvuto wowote ule na wakati mwingine huhatarisha hata usalama wa watumiaji barabara

2) Uvunjaji wa sheria za barabarani kila mahala na kila wakati. Watu wanatanua bila sababu ya msingi, waajiriwa wa majeshi ya ulinzi, polisi, kampuni binafsi za ulinzi kujiona wako juu ya sheria za barabarani, kero za misafara ya viongozi, watu kuegesha vyombo vyao vya usafiri kila mahala hata kwenye kona, pikipiki za BAJAJ- Uendeshaji wao na maegesho yao yasiyo rasmi, watu kutoheshimu makutano ya barabara na mizunguko (kipu lefti) hususan pale kwenye makutano ya Mwenge na Sam Nujoma, kutokuheshimu taa za kuongozea magari na waenda kwa miguu, watu kujivukia vukia hovyo tu barabarani, matuta kwenye dual carriage way na interstate highways, n.k
 
Bajaj bila kuuandaa infrastructure...
Frame za maduka KILA KONA ya mji...
Marundo ya uchafu kila sehemu
......
 
Back
Top Bottom