Nishaurini kuhusu huyu dada

Nishaurini kuhusu huyu dada

Mzee wa Masauti

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Posts
2,199
Reaction score
2,514
Sabalkheri wanajamvi wa MMU.

Nimekuwa msomaji wa uzi mbalimbali katika jukwaa hili lakini ni mara chache sana nimekua nikitoa mada.

Leo nina kisa kimoja ambacho ningeomba mnishauri wanajamvi, Ni hivi kuna mdada mmoja nilianza kumfuatilia kwa maana ya kumtongoza yapata mwaka mmoja na nusu umepita. Awali tulikuwa tunawasiliana vizuri kwa simu kwa miezi minne ya mwanzo na aliniambia yupo single by that time.

Kiukweli ni mdada alieumbwa akaumbika mashaallah. Lakini baada ya hapo ikawa kila nikimpigia simu hapokei au sometimes ananikatia na wala hajibu sms zangu kwa zaidi ya miezi nane hadi ikafika mahala nikakata tamaa kwa huyu bidada shosti.

Nilivyoona hali ngumu nawasiliana na mtu ambae ha-respond kwa chochote nikaamua kumpotezea.

Sasa mwezi uliopita yaani september picha likaanza tena. Baada ya kurudi zangu safari Dar kutoka Arusha nikawa nimelala zangu home ile naamka tu kucheki simu yangu nikakuta missed call yake. Wallah moyo ukashtuka kwanza mana nilijua hata namba yangu alishafuta kwenye contacts zake, So nikaamua kumpigia simu nijue kulikoni?

Basi nikamwendea hewani akapokea simu tukapiga stori za hapa na pale. Nikawa naweka bidii kwenye kuwasiliana nae akawa anapokea simu. Nikaanza kumkumbushia lile ombi langu akaanza kuniambia mara ooh nina boyfriend mara ooh hapendi kuwa nawasiliana nae.

sasa mi nikawa najiuliza kama ana mtu mbona ni yeye ndo alieanzisha mara baada ya kuyasitisha mwenyewe na yeye anajua kwamba kweli ninampenda na actually nilimuahi ninahitaji kumuoa.

Wajameni can i move on with that gal au nimpotezee mana nashindwa kumwelewa kabisa.

Ushauri tafadhali.


KING OF THE BEST MELODY
 
kwanini uruhusu mtu achezee hisia zako kiasi hicho
 
Nakushauri uachane nae kwasababu;
1. Hana mapenzi na wewe kwasababu ana mtu wake anayempenda kwa dhati.
2. Siku akikutafta ujue wamekorofishana na mtu wake kwahiyo anatafta faraja tu ya muda ingawa hawawezi kuachana.
3. You cant be lovers but u can be friends.
 
Taja jina lako kamili na yeye ntajie jina lake kamili nufanye mambo nipo pangan kwa siku saba nimekuja kumtembelea babu yangu
 
Hivi kwa nini mnapendaga single click? yaani mdada akikuzungushwa kidogo tu tayari umeishakata tamaa na kuanza kulalamika. Hebu komaa huko bana chukua huyo mtoto jumla jumla kama kweli unampenda kwa dhati.

Yaani umri huo unategemea kweli asiwe na mtu, yaani awe tu anakusubiri wewe, seriously? tatizo mnapenda kudanganywa ndo maana
 
Nakushauri uachane nae kwasababu;
1. Hana mapenzi na wewe kwasababu ana mtu wake anayempenda kwa dhati.
2. Siku akikutafta ujue wamekorofishana na mtu wake kwahiyo anatafta faraja tu ya muda ingawa hawawezi kuachana.
3. You cant be lovers but u can be friends.

Point ya 1. sometimes haeleweki mara anasema ana mtu mara ooh hana
Point ya 3. hata huo urafiki alikuwa hautaki kabisa mana hata namba nilihisi alifuta kumbe anayo
 
Mkuu huyo anakufanya we wa akiba..Anataka siku kikiwaka huko alipo awe na sehemu ya kupumzikia..Cha msingi na we mfanye wa dharula..Endelea na mishe zako tu..Siku akijipendekeza kula mzigo zen huna habari

Duuh , nimekusoma sana tu mkuu
 
Wewe umegeuzwa zombie.....wewe sio first choice
lakini unawekwa just in case first choice akizingua arudi kwako
 
Taja jina lako kamili na yeye ntajie jina lake kamili nufanye mambo nipo pangan kwa siku saba nimekuja kumtembelea babu yangu

ebana mtoto si atadata sana mana naskia Pangani huko noma sana
 
Atakiheshimu saba huku oangani ni noma sana hapa nikimwambia babu anpeleke kwa washkaji zake aloschool nao wataalam ni balaa ye babu ndo inamu wao mkubwa wa msikiti hapa wamemueka wao wamemwambia we tuswalishe na kusomesha dini mengine tuachie sis
 
Back
Top Bottom