Kwanza kuhamia ukweni ni sahihi?
Kuhamia ukweni ukiwa na maana ya mkoa walipo wakwe zako au nyumba ya wakwezo?
Kama ni mkoa haina tatizo isipokuwa jiandae kwa ugeni wa kila mara na kuletewa shida za hapa na pale zinazohitaji chapaa
Kama ni nyumbani kwa wakwezo, hebu achana na huo mpango
Sehemu yoyote ya Tanzania hali ya maisha haipishani sana, muhimu uwe na shughuli ya kukuingizia kipato
Wapi pazuri pa kuhamishia familia na kuanzisha maisha kwa maana ya utulivu, usalama, huduma za kijamii, bei ya ardhi ubora wake hasa kwa kujenga kilimo na ufugaji n.k
Tatizo la Mbeya, sehemu kubwa ya maeneo karibu na mji watu walishanunua kama una mpango wa kujenga, labda ubahatike upate mtu anauza nyumba.
Otherwise, kuna maeneo pembezoni mwa mji kama Isyesye, Itua, Nsalagha, Uyole, Iyunga, Veta unaweza kupata kiwanja na maeneo hayo ni tulivu bado.
La hasha maeneo kama wataka kupanga basi jaribu kupita Block T, Sae, Nanenane, Iyunga na Jacaranda (sina hakika kama Jacaranda kuna nyumba za kupanga)
Sasa hata eneo ulilopo haujalitaja, sisi tutajuaje kama wapaswa kukokama huko huko au ushafikia wakati wa kuvunwa [emoji23]