Nishauri; biashara gani inamfaa kwa sifa hizi; | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nishauri; biashara gani inamfaa kwa sifa hizi;

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kichwa Ngumu, Oct 19, 2011.

 1. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hi JF Members;
  nimeoa na ni mtumishi wa umma; mke wangu ni mama wa nyumbani hana kazi yoyote.
  naamini nikimwezesha anaweza.
  sina kipato kikubwa sana lakini naweza kupata kama 1.5 milioni ili aanzishe biashara yoyote.
  naomba wana JF mnishauri ni biashara gani inaweza kufaa kwa mtaji huo
  thank you in advance
   
 2. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Tueleze Unaishi mkoa gani,intrest za Wife zitasaidia ktk kushauri type of business.
  i would suggest aende sido ,wanatoa training za kutengeneza
  1-Shampoo ,liquid soap production etc
  2 Food packaging
  3.Baking-Cake za Harusi ,party etc
   
 3. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2011
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mazingira na apendacho shemeji kama jamaa alivyopendekeza hapo juu pia na jamii inayowazunguuka,mkuu.
   
 4. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  mazingira ya biashara ni muhimu kuyafahamu kabla ya kuamua kufanya biashara mkuu
   
 5. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  muulize yeye napenda afanye nini?
   
 6. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa sasa naishi Mkoa wa Tanga, Wilaya ya Korogwe;
  kabla sijamuoa alikuwa ananunua nguo na kukopesha
  nitafuata ushauri wako tutavisit sido
   
 7. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  kama unapoishi pana sehemu kuna soko lenye watu wengi, hata duka la rejareja litamfaa ili mradi kuwe na uhakika wa kupata bidhaa kwa bei ya jumla. utafiti muhimu.
   
 8. c

  changman JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tembelea sido kama walivyokushauri na ucheki utakachokiona kinafaa. Ni kitu ambacho mkeo akipende kukifanya sio kumlazimisha cha kufanya.

  Kwa 1.5 million unaweza kuanzisha biashara kwa kuzingatia vifuatavyo:

  1. Ni biashara gani inayotoka sana ambayo unaweza kuanzisha kwa mtaji mdogo
  2. Fanya shughuli unayoipenda kwasababu ukiwa unafanya shughuli unayoipenda hata kama uko katika kipindi kigumu kibiashara unakuwa una motivation kuendelea kuifanya coz unaipenda.
  3. Angalia matatizo yanayoizunguka jamii unapoishi na kutafuta solution yake. Hapo unapata idea ya biashara manaake mi naamini biashara ni kuisaisia jamii nayo inakulipa kwa solution unayoipa.

  Biashara nazoweza kufikiria kwa haraka haraka ni hizi:

  1. Kuanzisha duka dogo la kuuza vocha za simu. Hizi ni bidhaa zinazotoka fasta
  2. Kwasasa kuna maeneo hawana umeme so wanategemea mishumaa. Anzisha biashara ya ketengeneza mishumaa nyumbani. Mtaji wake ni mdogo tofauti na watu wanavyofikiri. Jifunze kwa ku click hapa:

  http://www.youtube.com/watch?v=FmKa_XJArLY
  How to Make a Candle: Step-by-Step Instructions for an Easy Candle - YouTubeHome made candles part 1 - YouTube
  So nimekupa linki tatu wanatumia njia tofauti tofauti so chagua njia utakayoona inafaa au mix hizo techniques na kutengeneza ya kwako

  3. Nunua pikipiki ufanye bodaboda (nadhani hilo ndo neno lake).
  4. Anzisha biashara ya matofali ya kuchoma. Tafuta eneo mweke kijana awe anachoma matofali wewe unakuwa unaenda kutafuta wateja.

  Nadhani hizo zitakusaidia.
   
 9. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Duuuuuuu!!!!!!!!!! asante
   
 10. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  chang man ahsante
   
 11. c

  changman JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asante
   
 12. Z

  Ze Maza Member

  #12
  Oct 25, 2011
  Joined: Nov 14, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimeipenda hiyo ya boda boda au bajaji tatizo hizo pikipiki au bajaji zahitaji sh. ngapi kama mtaji.
   
Loading...