Nishati Mbadala kwa matumizi ya nyumbani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nishati Mbadala kwa matumizi ya nyumbani

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Tangawizi, Jan 16, 2011.

 1. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Baada ya kutembelea sehemu mbalimbali za nchi yetu, ni wazi tulipo sasa tumeshaka karibu miti yote kwa ajiri ya kutengenezea mkaa ambao unatumika kama nishati kwenye nyumba nyingi kuanzia vijiji mpaka mijini. Kwa bahati mbaya hatukukata miti kwa mipango endelevu ya kupanda mingine ili tusijefika sehemu tukawa hatuna miti kabisa ya kukata.
  Nimekaa na kujiuliza sana hivi nini itakuwa nishati mbadala kwa ajiri ya matumizi ya nyumbani, vijijini na hata mijini.
  Ilivyo leo, gas imeanza taratibu kushika kasi ingawa bado kuna vikwazo vingi katika kuhakikisha watu wengi zaidi wanaitumia kama chanzo cha nishati. Mfano, leo hii matumizi ya gas yamekuwa makubwa na storage ya LPG nchini ni kama zimebaki vilevile. Hii inapelekea gas kukosekana na kuishiwa kulangua mpaka kufikia bei ya juu sana. Wengi hatutaweza kuzimudu hizi bei kama zitaendelea hivi zilivyo.
  Makaa ya mawe yapo ingawa hatujui nini cha kufanya nayo, au bado tunapanga deal ya namna ya kuneemeka nayo kwa wale walio karibu na kitoweo hicho!
  Umeme sote tunajua jinsi unavyotumika kama sehemu ya kujitajirisha kwa haraka haraka kwa watu wenye mamlaka ingawa wananchi tunapata shida kubwa za mgao usiokoma.
  sasa jamani nishati ipi itakuwa ndio mbadala kwa matumizi ya nyumbani maana kwa speed hii ya kukata miti nina shaka kama tutafika mbali sana bila kujikuta tuna shida kubwa ya upatikanaji wa mkaa
   
 2. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kwa kweli umelonga mkuu nilitegemea gas iwe mkombozi wetu lakini balaa tupu imepanda cana umeme wala ctaki kuongelea akuna jinsi unaweza kutukomboa kwa habari ya makaa ya mawe kwa tanzania yetu cjui kama mafisadi watatuhurumia najua itakuwa njia ingine yakuwanyonya watanzania ila 2tafika
   
 3. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huko mkuu, mbele giza nene!!
   
 4. N

  Nataka Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Think hard the answer is on your problem
  1.nishati mbadala iliyokaribu na nyumba yako na sio songas au kidatu
  2.Matumizi ya nyumbani tu.
   
 5. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  nadhani nishati mbadala inaweza kutumika tu.kuna vitu vingi ambavyo vinaweza kufanya kazi badala ya mkaa.MAPUMBA YA MPUNGA. haya mapumba nimeona baadhi ya watu wanatumia kupikia yaani kuna majiko yanayotengenezwa kienyeji yanayo tumia mapumba.pia uchomaji wa matofali.
   
 6. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Msipasue vichwa vyenu bure
  nishati ni Umeme. Achana na mafisadi wanaotumia umeme kujinufaisha sasa hivi. Hilo ni jambo la muda mfupi. Muda si mrefu sana kila mtu atazalisha umeme wake mwenyewe au kununua anaozalisha jirani kwa bei ya maelewano!
  Makampuni makubwa ya kuzalisha umeme yatakufa kifo cha mende hivi karibuni!
  Kitu ambacho makampuni hayo hayaoni ni kasi kubwa sana ya maendeleo ya kitechnologia kwenye nyanjazote ikiwemo Umeme! na wao hawachukui hatua zozote kujihami na kwenda sambamba na maendeleo hayo, WAMEBWETEKA
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,325
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Nimejaribu kufanya hivyo na wala sioni njia.....bila umeme na gas, njia nyingine ni za kudumu kwenye mazingira yetu?
   
 8. deom2i

  deom2i Member

  #8
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna njia nyingi za nishati za mbadala kama,

  1.Biogas, inatokana na mbolea hasa ya ngome kutengeneza gesi, hii unaweza pikia amakuwasha taa za gesi. Ni rahisi pia kuinvest.
  2.Kuna solar, kutokana na miyozi ya jua, unaweza tumia kwa taa na hata kupikia kwa kutumia majiko ya sola. Bado technologia yake ni ghali sana kwa kununua mwanzoni.
  3.wind generator, kutokana na upepo kutengeneza umeme, hii inafanya kazi masaa wote na siku zote kwani upepo hausimami ikiwa juu bila kuzingwa. Hii technologia ni ghali pia kama solar na inaweza kutumika kwa taa na hata majiko kwa kupika.

  Hizi ndio ambazo tunaweza kutumia majumbani kwetu, tatizo ni pesa ya kununua kwanza, ila ukiweza tumia vifaa hivyo unasahau umeme wa mgao.
   
Loading...