Nishati kutenganishwa na madini: Pinda

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
Hoja ya wapinzani inaelekea kupita kwamba wizara ya Ngeleja kuelemewa na vyote nishati na madini.

Waziri mkuu sasa amekubali kwamba hili litapelekwa kwa rais kuangalia kutenganishwa wizara za MADINI na NISHATI.

Heko John Cheyo aliye_analyse kwamba hata hotuba ya Ngeleja ya leo ilitumia dakika 5 tu kwa madini.

Heko kambi nzima ya upinzani.
 
Juzi JK alisema suala la kugawanya Madini na Nishati limeshindikana sasa hivi kwa sababu ya bajeti iko mlangoni.

Kukaa kwetu kimya kunachangia hawa walale na waje sasa na kauli kana kwamba tulishasahau kuwa walishauriwa siku tele.
 
Yeah Sababu Rais Kikwete kasema Gas nyingi sana imepatikana na petroli karibuni itapatikana; kwahiyo ni lazima zitenganishwe

Cha kunishangaza ni aliposema Madini bado ni namba 2; baada ya Utalii ambayo ni namba 1; inayoipatia Nchi fedha za kigeni

Hapo alinitoa raha, Mwaka jana Dhahabu tu tulisafirisha ya Gharama ya Dola Billion 4.5 nchi ilikuwa ya Nne kwa kusafirisha Dhahabu barani Africa, ina Maana kwenye hizo Dola billiona 4.5 tulipata kama million 2 au 3; na Madini mengine kama Almasi, Coal n.k tulipata Dola mil 1? Ingekuwa bora kuyaacha ardhini kuliko kuwapa hao wazungu, uzuri tu wanaoa Wasichana wetu wa Kitanzania.
 
kwa hiyo mnachosema ni kua hii serikali haitekelezi chochote mpaka ipate pressure kutoka upinzani na kwa wananchi??
 
Yeah Sababu Rais Kikwete kasema Gas nyingi sana imepatikana na petroli karibuni itapatikana; kwahiyo ni lazima zitenganishwe

Cha kunishangaza ni aliposema Madini bado ni namba 2; baada ya Utalii ambayo ni namba 1; inayoipatia Nchi fedha za kigeni

Hapo alinitoa raha, Mwaka jana Dhahabu tu tulisafirisha ya Gharama ya Dola Billion 4.5 nchi ilikuwa ya Nne kwa kusafirisha Dhahabu barani Africa, ina Maana kwenye hizo Dola billiona 4.5 tulipata kama million 2 au 3; na Madini mengine kama Almasi, Coal n.k tulipata Dola mil 1? Ingekuwa bora kuyaacha ardhini kuliko kuwapa hao wazungu, uzuri tu wanaoa Wasichana wetu wa Kitanzania.
Analysis yako siielewi. Hujasema utalii uliingiza kiasi gani ili ulinganishe na madini na hatimaye raha kutoka.
 
Back
Top Bottom