Nishani kwa Polisi na Wanajeshi wa Westgate

Nishani kwa Polisi na Wanajeshi wa Westgate

KakaJambazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2009
Posts
18,830
Reaction score
12,314
Naomba kujua ka waliojitolea kuokoa maisha ya watu pale westgate wameitwa Ikulu na kutunikiwa nishani.
 
Naomba kujua ka waliojitolea kuokoa maisha ya watu pale westgate wameitwa Ikulu na kutunikiwa nishani.

Hivi yule kijana shujaa Abdul Haji mtoto wa Waziri wa Usalama mstaafu wa Kenya ambaye si mwanajeshi je atapata nishani hizo??? Ila big-up guy!!!
 
Waliokoa watu wangapi jamani na kukamata mashetani wangapi? Naomba mnifahamishe tu na wala sizuii nishani zao.
 
Mornie niliona on Tv Citizen Tv Wakiwaombea waliopoteza uhai kuumia na kuombea amani pia Kuwaambia Magaidi kuwa walidhania wakenya watatengana lakini ndio wamekuwa wamoja zaidi... Wakuu wa dini Viongozi na Raisi walikuwepo pamoja na watoto .... Ila lugha yao kuu ilikuwa ni English. Arabic, Hindi na Hindu zilikuwa ni kwa ajili ya Dua tu. Shehe pekee aliongea Kwa Kiswahili bila kugusa neno lolote la English!
 
Hakuna hata gaidi aliyekamatwa wala kuuawa! waliacha wame-set milipuko nao wakajifanya wanatoka kama mateka! waafrika tunachangamoto ya kukabiliana na magaidi coz huwezi kutofautisha kati ya gaidi na mtu wa kawaida
 
Waliokoa watu wangapi jamani
na kukamata mashetani wangapi? Naomba mnifahamishe tu na wala sizuii
nishani zao.
kaka hakuna askari wakupewa nishari pale wanajeshi waliingia na kuvunja mabenk na masonara ndo sababu walichukua uamuzi wa kulipua jengo harakax2
 
Hivi yule kijana shujaa Abdul Haji mtoto wa Waziri wa Usalama mstaafu wa Kenya ambaye si mwanajeshi je atapata nishani hizo??? Ila big-up guy!!!
Huyu jamaa Abdul Haji alijipanga ili apate sifa. Kati ya watu wasiostahili kupata nishani ni huyo. Kwanini Camera ikufuate wewe pekee? Au anaishi kwenye 3D. Alikuwa anatengeneza jina...
 
Naomba kujua ka waliojitolea kuokoa maisha ya watu pale westgate wameitwa Ikulu na kutunikiwa nishani.

Waitwe Ikulu na kutunukiwa nishani kwa ushujaa gani walioufanya? Uchunguzi bado unaendelea............!!!
 
Huyu jamaa Abdul Haji alijipanga ili apate sifa. Kati ya watu wasiostahili kupata nishani ni huyo. Kwanini Camera ikufuate wewe pekee? Au anaishi kwenye 3D. Alikuwa anatengeneza jina...

Mimi mwenyewe kwa kweli simuelewi Abdul Haji na kamwe sitomuelewa..camera inamfuata yeye 2. Hana Bullet proof 3.Milio inayotoka ndani ni mikubwa ukilinganisha na kale kabastola kake alikokashika kizembe tuu 4. yeye pia ni msomali

Ningekuwa Inteligence Officer .."i could have gone one mile far to know what kind of this man" haya ni mawazo yangu tu ya kiraiaraia msinitukane plsss.
 
Huyu jamaa Abdul Haji alijipanga ili apate sifa. Kati ya watu wasiostahili kupata nishani ni huyo. Kwanini Camera ikufuate wewe pekee? Au anaishi kwenye 3D. Alikuwa anatengeneza jina...

Kwa hiyo unataka kusema alijua kama kuna ugaidi utatokea katika jengo hilo na kujiandaa kwa kuwa na mtu aliyekuwa anampiga picha? Yataka moyo wa kizalendo na kishujaa kufanya yale aliyoyafanya Abdul Haji!
 
Mbona kwetu wale wa ghorofa walipewa nishani?

Ni kazi gani ambazo ziko kwenye hadidu za rejea za kazi zao ambazo ndiyo sababu ya mishahara yao na maana halisi ya ajira yao na ni kipi kilichobzidi hapo ambacho hawa watu (askari) wa kenya wapewe nishani? Na kwa nini wamekuwa wakitoa taarifa za uwongo uwongo kweny public juu ya watu waliopoteza maisha na juu ya haya mashetani? Baada ya kazi yenye zero impact, wanapewa nishani ya nini jamani? Mbona hizi nishani zimekaa kisiasa siasa na kishikaji shikaji kama si kikijiweni kijiweni sana?
 
Hawa wa Tanuzania kupewa nishan i huwa ni malengo ya kisiasa zaidi. Wewe umeajiri kikosi cha uokoaji na unawalipa kwa hiyo. Wanapocharge kazi zao za kuokoa unawapa nishani bila hata kufikiria kipi kimezidi kiwango chao cha kazi kinachotakiwa. Kumbe walitakiwa wasiokoe? Na kumbe kazi yao n ini? Hizi nisani usu, zinapalilia mazingira ya kukosa uwajibikaji kazini na rushwa!.

Nishani zitolewe pale mtu kafanya zaidi ya kiwango cha kawaida kinachotarajiwa. Siyo hovyo hovyo tu kupeana rushwa na kampeni za kishikaji.
 
Back
Top Bottom