Nisajili Nini Kati ya Kampuni na Jina la Biashara?

Nisajili Nini Kati ya Kampuni na Jina la Biashara?

Luhamba II

Senior Member
Joined
Mar 22, 2025
Posts
137
Reaction score
219
Hili ni swali nililoulizwa na dada anaitwa "Lahey" juzi majira ya Saa 10:45 hivi jioni.

Actually hii ni mara ya 17 naulizwa hili swali ndani ya miezi miwili.

Na jibu langu hua ni moja tuu kila ninapoulizwa hili swali.

"Sajili Kampuni"

Hua Nina sababu kadha wa kadha ambazo hua Zinafanya nitoe hili jibu, Leo nitakutajia tatu;

1. Liabilities
Liabilities za Kampuni mfano madeni yanabaki kua madeni ya Kampuni tuu.
Wadai wako hawaruhusiwi kuzuia personal account yako au kugusa mfuko wako binafsi.

Ukiwa na biashara au jina la biashara madeni ya biashara yako ni madeni yako pia, person saving account inaweza tumika kulipa hayo madeni.

2. Taxes (Kodi)
Ukiwa na Kampuni na ukapata hasara au break even hautalipa Kodi.

Sheria za makampuni zinakuruhusu ku file uneven losses kwa miaka miwili mfululizo na usilipe Kodi.

Lakini pia ukiwa na Kampuni Kodi inakatwa kutoka kwenye faida na sio makadirio.
Hii Ina maanisha pesa ya mtaji na Mikopo haziguswi kabisa.

Hii privilege huwezi pata kwa kusajili jina la biashara.

3. Mitaji
Ni rahisi ku access mitaji ukiwa na Kampuni mfano

-Unaweza kuuza hisa za Kampuni na ukapata mtaji wa kuendeleza biashara.

-Unaweza kupata mikopo kutoka kwa watu binafsi na taasisi za kifedha.

Bonus Tip
Watu wengi wanaamini Kuna transparency kubwa sana kwenye Kampuni kuliko biashara binafsi, hivyo ni rahisi kupata TRUST kutoka taasisi za kifedha na watu binafsi.

Hey, naitwa Luhamba Mimi ni mwanasheria na agency freelancer, nawasaidia wafanya biashara kama wewe kusajili biashara leseni na Kampuni.

Kama unahitaji consultation zaidi kuhusu usajili wa Kampuni biashara leseni, trademark na patents unaweza kunitumia ujumbe WhatsApp kupitia namba hizi

0678131068

Your Favorite Lawyer.
 
Kuhusu deni la kampuni kutohusishwa na mwenye kampuni hapa inategemea. Taasisi nyingine kama benki au wakopeshaji wa bidhaa huwa wanataka dhamana yako binafsi juu ya hiyo ya kampuni. Wengi watu huja kugundua mtego huu baada ya kuarifiwa walipe deni.
 
Kuhusu deni la kampuni kutohusishwa na mwenye kampuni hapa inategemea. Taasisi nyingine kama benki au wakopeshaji wa bidhaa huwa wanataka dhamana yako binafsi juu ya hiyo ya kampuni. Wengi watu huja kugundua mtego huu baada ya kuarifiwa walipe deni.
Inategemea kama Kampuni Haina assets za kutosha kudhamini mkopo.

Hata hvo hawatakurupuka tuu, Kuna process inaitwa waiver.
 
Waiver ni nn?
Kampuni kisheria ni mtu, kwahiyo madeni ni ya Kampuni sio yako Mmiliki.
Sasa waiver, ni Hali ambayo Sheria inaacha kupambana na Kampuni inaanza kukuangalia na wewe binafsi kama Mmiliki wa Kampuni.

Hii hutokea mara chache ikiwa utadhulumu watu wa mgongo wa Kampuni, kuuza vitu haramu kwenye Kampuni na sababu kama hizo.

Ambapo hapa sasa unaweza shitakiwa wewe binafsi au akaunti zako kushikiliwa.

Ila mpaka unafikia hapa maana ake umekithiri.
 
Back
Top Bottom