Nisaidieni upelelezi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nisaidieni upelelezi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ziroseventytwo, Sep 30, 2012.

 1. Ziroseventytwo

  Ziroseventytwo JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 3,522
  Likes Received: 1,515
  Trophy Points: 280
  Tarehe 18/09/2012 kulitokea wizi wa mzigo wenye thamani ya tsh 15000000/=. Mzigo huo(mchele) ulipakiwa ifakara kwenye gari no T 414 BXD mitsubishi fuso likiendeshwa na mtu aliyetambulika kama Kelvini komba. Siku ya tukio kulikuwa na gari mbili zote fuso, rangi zinafanana, na zote zinatumia no T 414 BXD, baada ya gari zote kuondoka hapa, walipofika kwenye geti,gari moja inaonyesha imepita kwa kutumia namba hiyo hapo juu. Lakini 1 halikupita. Tumeangalia mizani, ya mikumi, mikese na kibaha gari iliyopita ni hiyo moja tu. Tukachukua namba za magari zilizopita pale getini kwa siku hiyo na kuzipeleka TRA, Namba moja inaonyesha ni ya pikipiki, na mmiliki wake yupo Tanga. Na hii ambayo ina namba ya pikipiki haijapita mizani hata m1.T 414 BXD mmiliki wa gari yupo makambako. Tulipofika makambako, mmiliki wa gari tulimkuta na gari pamoja na dereva wake.. Namba ni ile ile inayotuhumiwa, rangi ileile tofauti ni cabin. Inayotuhumiwa c cabin mayai. Hii ya makambako wanakubali kweli walipakia mzigo hapa ifakara, lakini walifikisha. Na mwenye mzigo anakiri kupokea mzigo wake. Namba ya simu ya dereva aliyepotea na mzigo imesajiliwa kwa jina la kelvin komba. Hata leseni yake ina jina hilo. Mpaka sasa madalali waliopakia wamefunguliwa mashtaka ya wizi wa kuaminiwa.(ingawa hawaelewi chochote) ndg zangu hebu nisaidieni kuunganisha dot tuweze kumpata mwizi wetu.
   
 2. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,532
  Likes Received: 1,020
  Trophy Points: 280
  Duu, huu mchezo ulochezwa hapo ni wa KIMAFIA,
  anyway ngoja nianze taratibu kufuatilia POST yako.
   
Loading...