Nisaidieni tafadhali....!

Sadma

Member
Sep 10, 2011
20
4
Nilijifungua 2008 kwa kisu so sikuweza kulifunga tumbo bcoz ya kidonda cha operation, sinc then tumbo langu ni kubwa , nifanye nini ili kulipunguza?Maana hata nguo hazikai fresh mwilini shauri ya tumbo. Nisaidieni pls
 

mikatabafeki

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
12,790
4,621
chukua ile mikanda ya polisi uwe unajifunga lakini jitahidi kukaza hadi uhakikishe ushuzi unakua unatoka
 

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,902
3,077
Duh, pole sana ndugu! Jaribu kuchek ushauri wa madaktari. Hapa JF kuna watu hawajui what is bioz wanaweza kukudanganya tu. Kachek wataalam.
 

Likwanda

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
3,914
1,115
Chukua ushauri wa kwenda hospital, huko watakupatia njia salama zaidi ya tatizo lako.
 

Pretty

JF-Expert Member
Mar 19, 2009
2,575
535
.......Mie nadhani tatizo sio kufunga tumbo, ila ulikuwa una kula kula sana, na mazoezi hufanyi.
Hata mimi nilipata c- section lakini tumbo na mwili wangu umerudi kawaida .......baada ya miezi 3 tokea nijifungue nikaanza kufanya mazoezi na kula matunda, mboga mboga na maji kwa wingi. Kama unakula kuku usile ngozi na punguza kula nyama nyekundu.

Hata sasa kama unataka kuondoa hilo tumbo unaweza kabisa, usiwe una kula kula bila mpango. Na uwe makini nini unakula, sio kila chakula uingize tumboni.
 

Sadma

Member
Sep 10, 2011
20
4
.......Mie nadhani tatizo sio kufunga tumbo, ila ulikuwa una kula kula sana, na mazoezi hufanyi.
Hata mimi nilipata c- section lakini tumbo na mwili wangu umerudi kawaida .......baada ya miezi 3 tokea nijifungue nikaanza kufanya mazoezi na kula matunda, mboga mboga na maji kwa wingi. Kama unakula kuku usile ngozi na punguza kula nyama nyekundu.

Hata sasa kama unataka kuondoa hilo tumbo unaweza kabisa, usiwe una kula kula bila mpango. Na uwe makini nini unakula, sio kila chakula uingize tumboni.
Kiukweli niikuwa nakula bila mpango, Thanx kwa ushauri nitaufanyia kazi
 

Riwa

JF-Expert Member
Oct 11, 2007
2,597
3,018
Kiukweli niikuwa nakula bila mpango, Thanx kwa ushauri nitaufanyia kazi

Pole Sadma...Kiukweli wanawake wengi huwa wanapotoka na ile dhana nzima ya kufunga tumbo. Unapojifungua kuna matumbo mawili inayobidi yarudi. 1; Tumbo la uzazi (yaani kizazi chenyewe). Size ya kizazi katika hali ya kawaida hakizidi size ya mpira wa golf, lakini wakati wa ujauzito you can imagine kinavyotanuka na kujaa. Baadaya kujifungua kizazi huwa kinarudi taratibu, na kinapofanya hivyo ndio unapunguza upotevu wa damu na kuongeza kasi ya utokaji wa yale maji maji ya arobaini (lochia). Kufunga tumbo husaidia kizazi kurudi haraka, lakini hata usipofunga (mara nyingi kwa waliojifungua kwa operation) kizazi hakitabaki kikubwa, kitarudi tuu mpaka size yake hiyo ndogo. 2; Tumbo la nje (abdominal wall). Wakati wa ujauzito tumbo la nje au ukuta wa tumbo nao uvutika ili kuweza kuaccomodate kizazi kinavyopanuka kadri mtoto anavyokuwa, na ndio maana wakati mwingine wanawake huwa wanapata zile stretch marks iwapo nguzi inavutika sana au kwa kasi sana. Lakini pia, kikubwa ni kuwa wakati wa ujauzito mama hula sana ili mimba iweze kukua vizuri, hii nayo inaongeza kujaza mafuta kwenye ukuta wa tumbo. Unapojifungua na kizazi kurudi chenyewe au kwa kufunga, tumbo la nje au ukuta wa tumbo nao unarudi lakini taratibu sana kuinganisha na kurudi kwa kizazi. Na uwepo wa mafuta huchelewesha zaidi tumbo la nje kurudi, na wala kufunga tumbo hakusaidii tumbo la nje kurudi ( bali tumbo la uzazi tu).

Mara nyingi tena baada ya kujifungua wanawake wengi wanakula sana ili kutoa maziwa ya kutosha, hii inaendelea kujaza mafuta kwenye tumbo la nje/ukuta wa tumbo..na kufanya lisirudi bali kuvimba zaidi!

Kama alivyokushauri dada Pretty, tumbo hili njia pekee ya kulipunguza/kuliondoa ni kwa kufanya diet (kama umemaliza kunyonyesha) na zaidi ni kufanya mazoezi ili kuchoma mafuta yaliyojazana hapo tumboni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom