nisaidieni nifanyeje kuhusu gf wangu!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nisaidieni nifanyeje kuhusu gf wangu!!!!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by msani, Nov 6, 2011.

 1. msani

  msani JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  habari zenu wana mmu.
  leo nimekutwa na tukio ambalo sijajua tatizo ni nini na nifanye,
  nina gf wangu ambaye kwa sasa yuko kwao nje ya mkoa,na kipindi fulani tulikuwa na matatizo ya mawasiliano baina yetu maana alikuwa hapokei simu mara nyingi ninapompigia,baadae nikaanza kuhisi huenda ana jamaa huko.Tukakwaruzana na baadaye tukasuruhisha na tatizo la simu likapungua kwa asilimia kubwa.Nilikuwa nafahamiana na mdogo wake na muda mwingi nilikuwa naongea naye akinipigia kwani mie kupiga mara kwa mara niliona sio vizuri na inaweza hatarisha mahusiano yetu.Huyu mdogo mtu akawa ananiambia mara kwa mara kuwa huyu mwenzangu sio mwaminifu kwangu anapokuwa nyumbani na akanikumbusha mgogoro wa simu na kuwa kuna jamaa ambapo si mmoja huwa anamtoa mara nyingi na kurudi nyumbani usiku wakati mwingine hata saa sita usiku.Kuna siku aliniambia kuwa jana dada alitoka na jamaa na kurudi saa tano usiku lkn mie mara nyingi takribani kila siku tunaongea naye na ananiambia yuko nyumbani usiku huo,nikakasirika sana baada ya kuambiwa na mdogo mtu hiyo taarifa ila nikajisemea moyoni nisifanye pupa.Leo 5/11/2011 saa 3 usiku mdogo mtu akanipigia simu tukaongea tu kwa muda wa dk 15 na baadae mada ya dada ikagusiwa nami nikataka kujua zaidi,akanisimulia halafu akasema hata leo hayupo nyumbani na ametoka na jamaaa fulani.kijana jazba ikanipanda na kwa kuwa natumia simu 2 nikapiga na simu ya pili huku tukiongea na mdogo mtu,uzuri gf wangu akapokea simu na kumuuliza kama ananipenda na akajibu ananipenda,nikamuuliza tena mara ya pili akaanza kulia,ndipo nilipomuuliza yuko wapi na akaniambia yuko nyumbani na akawa amepaniki na kumuita modgo wake ili nithibitishe kama ni kweli niko home na akamuita mdogo kwa sauti ya juu na huku nikisia,nikakata simu ya mdogo mtu,baadaye gf wangu akaniambia huyu hapa ongea naye,nikazuga kidogo kisha akampa gf wangu simu huku akilia sana kwa swali nililomuuliza na kumtuhumu kuwa hayuko nyumbani.
  sasa nimeshindwa kuelewa nini kinaendelea na lipi ni kweli maana leo gf alikuwa nyumbani na nimeambiwa kuwa ametoka na nifanyeje angalau niweze kujua ukweli kwani mi niko mbali kwani nashindwa tena kumwamini mdogo mtu, na nahisi naibiwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 2. R

  RONALDO Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana kaka kwa mkasa wako huu mm nakushauri ucwe na pupa kaa na ufanye research ya polepole kuhusu huyo mdogo wake demu wako yawezekana hapend kuona mpo pamoja na vilvile mchunguze na huyo demu wako polepole pacpo pupa
   
 3. msani

  msani JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  asante mkuu nitalifanyia kazi
   
 4. C

  CYPRIAN MKALI Senior Member

  #4
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  huyo dodo labda hapendi uhusiano wako na dadake, so kama ingekuwa mwizi leo ndio ilikuwa 40 yake. sijui labda ndo aliingia time hizo hivyo ikawa bahati kwake.
  la msingi wewe jipe matumaini ni mwaminifu ili uendelee vizuri na mambo yako, tofauti na hapo utakosa gf na mambo yataharibika.
  mahusiano ya mbali hayahitaji wivu, hakika itakugharimu muda na pesa na unaweza punguza pendo wivu ukizidi mwisho unapoteza.
  ila mkikutana tena ikiwezekana mjikinge halafu mpime ngoma kama ulikuwa unaenda kavu ndo mambo mengine yafuate.
  piga kazi kaka wewe muamini itampa nguvu hata yeye na kama anagawa utajua, hakuna marefu yasiyo na ncha.
   
 5. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  Pole sana jamaa angu! Inaonyesha kwa research ndogo ya maelezo yako, kwamba mdogo mtu hapendi mahusiano yenu,na sidhani kama mpenz wako anakucheat mana kama ni m2 ambaye anakucheat hawez kulia ,mana atakuw ameshakutoa moyon mwake.. Hapa itakuwa mdogo m2 anakutaka wewe na anafanya mbinu zote ili akupate.au hapend mahusiano yenu. Ndo mana anakupa visa vya UONGO ili umwone Mpeny wako mcharuko.. Kwa ushauri kama unatak kutambua ukweli,fanya hivi. Kila anapokupigia mdogo m2 jaribu pia kumpigia mpenz wako ili ubaini ukweli, na kama ukigundua ni Mdogo m2 ni Mwongo, si vibaya kama ukamshirikisha Mwenzi wako.
   
 6. msani

  msani JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  nimekuelewa sana mkubwa,ila hapo kwenye palinisumbua sana baada ya yeye kusema yupo nyumbani na hapo kwenye red sijawahi kuuza mechi ndg yangu ila nashukuru kwa ushauri wako na nitafanyia kazi,asante sana
   
 7. msani

  msani JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  asante kwa ushauri mkuu lkn hapo kwenye red ndo ameishanitoa moyoni kwa kulia ama?
   
 8. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,978
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  mwana wewe wala hamna shida ya kufanya research hapa maana utajipa mahangaiko ya bure
  sasa hapa hamna tena mahusiano...so chukuwa hamsini zako na tulia pembeni....fimbo ya mbali haiui nyoka!!!!
   
 9. msani

  msani JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  kwahiyo mzabzab ndo nimuache?
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  This story is rated 8yrs.
   
 11. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #11
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Sasa akijua wakati ikiwa too late je? Lifanyie kazi mwaya kha!
   
 12. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #12
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Soko huria limeharibu mapenzi
   
 13. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #13
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  blue and bolded: jamaa yangu we ndo lofa kweli, unawajua wanawake wewe?
   
 14. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #14
  Nov 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  what if mdogo mtu naye anataka? Familia nyingine watoto adabu zero. Ktk hili mi nnachoona ni kama mdogo mtu naye anataka hivyo plan yake ni 'kupindua nchi hapo'.
   
 15. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #15
  Nov 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,119
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  mi nahisi alilia kukuvuta zaid coz cku hiyo alikuwepo home ka vip muwekee GPS.
   
 16. imma.one

  imma.one JF-Expert Member

  #16
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 545
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Du pole sana,ila jitahidi kuhakikisha kama kweli ni bora usepe
   
 17. m

  majogajo JF-Expert Member

  #17
  Nov 6, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  mwambie mke wako arudi nyumbani kwake mapema.
   
 18. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #18
  Nov 6, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ukitaka kujua ukweli zaidi mtongoze huyo mdogo wake na akikukubali jua kuwa uyo dogo ni mbea na alikuwa anakutaka wewe ila dada yake sio kicheche
   
 19. d

  december Member

  #19
  Nov 6, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana mkuu.wanawake wa siku hizi ni pasua kichwa, vumilia tu ni mapito.ushauri:fanya uchunguzi kwa makini kabla hujachukua maamuzi ya kummwaga kabisa.lakini kabla ya kummwaga, 'piga' kabisa na mdogo wake ili kupunguza machungu!!!
   
 20. msani

  msani JF-Expert Member

  #20
  Nov 6, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  hapo si ndo nitaharibu kabisa,asante
   
Loading...