Mimi ni mwanaume,
Nimefikiria sana mambo mengi, nimepitia uzoefu mgumu sana maishani, kijamii na kimahusiano.
Kimaisha (uchumi) sijafeli sana, niko vizuri. Ila kwa changamoto nilizopitia, nimekuwa na mtazamo tofauti kuhusu maisha.
Nimejikuta nachukia wanawake kuliko maelezo, nikimwona mwanamke naona kama jambazi anapita pembeni yangu.
Nimejawa na roho ya ukatili na kisasi. Kitu kinachoitwa mapenzi kwangu ni kama hadithi (myth).
Nilipogundua hali yangu nikaamua kuwa busy na shughuli za kiuchumi, lakini naona hakuna nafuu. Siwezi kueleza yote hapa nishaurini nifanyeje nirudishe ubinadamu wangu na furaha yangu. Naumia sana
Updates!!!!
Nashukuru kwa ushauri, kejeli na mitazamo yenu.
Kwa ujumla Mambo yaliyoniumiza sana katika maisha yangu ni;

- Ndoa haiko vizuri. Matarajio yangu kwa niliyempenda na nilivyokuwa namfahamu, yamegeuka kuwa jehanamu ndogo. Sina furaha wala hamu tena, ninapotazama nyuma na nilipo, majuto yananiumiza. Sometimes nawaza kuwa nilifanya makosa fulani katika kufanya maamuzi, sasa ndo yananigharimu.
- Pale nilipoamua kujiliwaza kwa kutafuta relief kwingine kila mara huishia kwa maumivu zaidi kuliko faraja. Maumivu ya kutendwa ni afadhali ya jana.
- Sioni faida ya elimu yangu niliyoisotea muda mrefu, wala mali ninazomiliki.
- Nimegundua ni vigumu sana kumweleza rafiki wa karibu sana ambaye unadhani ni msaada, kumbe ni wanafiki. Sasa kubaki na majipu moyoni naona nakaribisha kifo bila kujielewa.