nisaidieni jinsi ya kumshauri: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

nisaidieni jinsi ya kumshauri:

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mrs Patrick, Sep 17, 2012.

 1. M

  Mrs Patrick Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nina rafiki yangu amekuja kuomba ushauri: ana mpenzi wake wana uhusiano wa mwaka mmoja. wanaishi mbalimbali, na tangu waanze uhusiano wameonana mara mbili tu ambayo ni mwezi wa kumi mwaka jana na mwezi wa kwanza mwaka huu.ila mwanzoni mwa uhusiano wao mkaka alikuwa anampigia simu sana, walikuwa wanachat pia. ila tatizo linakuja ni kwamba saiv yule mkaka kabadilika. mara ya mwisho wameonana ni january, na mpaka sasa hawajaonana. na hata walivyoonana alikuta message za wasichana wengine, ila huyo mkaka akasema hao wadada ndo wanamtaka.sasa rafiki yangu akimwambia waonane, mkaka anasema yupo busy na shule. saiv shule kamaliza lakini anatoa visingizio kibao. na pia mara nyingi hapatikani kwenye simu anasema sehemu aliyopo kuna shida ya umeme. sasa anashindwa kumuelewa mpenzi wake huyo, nimshauri vipi jamani.
   
 2. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  mwambie amuache!haya maisha mafupi jamani hayo ndo kwanza urafiki,!cha kufia nini bana!
   
 3. Eversmilin Gal

  Eversmilin Gal JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 783
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ajaribu kuwa kimya ka miezi miwili hamna kupiga simu wala kutuma text aone upande wa pili utarespond vip
   
 4. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,200
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Urafiki wa mwaka mmoja tena wa kuona mara mbili tu nao unahitaji ushauri? Ndoa za miaka 20 zinavunjika bila ushauri itakuwa urafiki? Kwangu mimi naona sio dhambi huu urafiki ukivunjika for good!! Aanze upya tu lakini awe makini asijekurupuka akakanyaga ****
   
 5. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,395
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Haya mapenzi mbona balaaa,kila kukicha katendwa au katenda,server inajaa jamani.

  Back to topic
  Mpe pole sana mwambie fimbo ya mbali haiui nyoka
   
 6. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  hivi watu mbona bado wana ng'ang'ania mapenzi ya long distance wakati inaonekana kabisa kuwa haya dumu?
   
 7. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,334
  Likes Received: 2,648
  Trophy Points: 280
  ukiona manyoya ujue imeliwa...kwa nini kujiumiza moyi kwa mtu ambaye sio baba, kaka wala ndugu...piga chini endelea na maisha mengine...wanawake bhana wanaume wengine huwa wanaamini mwanamke ukiona visa vinaanza kama hivyo utakuwa ushapata mustakabali wa nini kinaendelea lakini wadada huwa mnakuwa wagumu kuelewa
   
 8. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  ushauri wa nini wakati lipo wazi, me najua kama unampenda mtu kila unapopumzika lazima umuwaze na lazima umpigie kila siku, ukishindwa kabisa haziwezi kupita siku mbili...othrwz no love...akate kona
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Huyo alikuwa anataka kipapaa tu, keshapata anaendelea kutegua mitego mingine. Muambie aamini mtima wake. Hana hata majirani wa majirani zake jamani?
   
 10. piper

  piper JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ukiona manyoya ujue ......................? nafikiri kwa hapo utajaza mwenyewe, mwambie rafikiyo akimbie kungali mapema
   
 11. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mwambie akae humu.
   
 12. jamiif

  jamiif JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 2,417
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  ushauri wa kufuatwa ni huu wa mkuu Gerrard tu!
   
Loading...