Nisaidieni huyu mwanamke ananisumbua!

Mibas

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
4,168
6,291
Habari zenu,

mimi na huyu mwanamke tuko hapa Aman-Jordan tumefika hapa mchana tukitokea dubai tulipokutania yeye akitokea Dar alinikuta Dubai kwa vile yeye aliniambia nitangulie ili nimtafutie sehemu atakapopata bidhaa anazohitaji kwa ajili ya biashara zake za nguo na cosmetics. Gharama zote amenilipia: Transport, Accomodation na matumizi mengine tunapokua safarini analipa yeye mimi amenichukua kwa malipo ili nimsaidie Translation yeye hajui kiingereza vizuri na kiarabu hajui kabisa na hizo ndizo lugha watu wengi hapa wanatumia. Sasa tatizo ni kwamba sasa hivi anakataa kulala chumbani kwake eti anaona vitu kama mashetani chumbani kwake mimi nikienda pale sioni kitu. Anasema lazima alale chumbani kwangu naogopa kukataa kwa vile hela yangu amenilipa nusu tu na balance mpaka nikimaliza kazi next tuesday. Naomba ushauri nimkimbie au nisubiri nione kama kesho atarudia tabia hii.

Asanteni.
 
Haina shida lalanae tu,kama kuna jingne si utajua? Ikibid kila mtu ktanda chake,kama ni kmoja wewe chin yeye juu!
 
Lala chini mkuu usilale nae kitanda kimoja litakuwa kosa kubwa sana
 
tayari keshalala kitandani na mimi ndo nataka nilale chini bahati nzuri kuna carpet nzito.
 
Uwe makini wengine wanatafuta wa kuwaachia virusi kabla hawajatangulia. Jali maisha yako ya baadae ni bora kuliko vijisenti vya leo.
 
Kwani ni mamako au dadako? Kama si ndugu yako kinachokufikirisha ni nini? Mpe anachotaka, kwani itakugharimu nini? Au utatakiwa kulipia baada ya kufanya anachotaka ufanye?
 
Habari zenu,

mimi na huyu mwanamke tuko hapa Aman-Jordan tumefika hapa mchana tukitokea dubai tulipokutania yeye akitokea Dar alinikuta Dubai kwa vile yeye aliniambia nitangulie ili nimtafutie sehemu atakapopata bidhaa anazohitaji kwa ajili ya biashara zake za nguo na cosmetics. Gharama zote amenilipia: Transport, Accomodation na matumizi mengine tunapokua safarini analipa yeye mimi amenichukua kwa malipo ili nimsaidie Translation yeye hajui kiingereza vizuri na kiarabu hajui kabisa na hizo ndizo lugha watu wengi hapa wanatumia. Sasa tatizo ni kwamba sasa hivi anakataa kulala chumbani kwake eti anaona vitu kama mashetani chumbani kwake mimi nikienda pale sioni kitu. Anasema lazima alale chumbani kwangu naogopa kukataa kwa vile hela yangu amenilipa nusu tu na balance mpaka nikimaliza kazi next tuesday. Naomba ushauri nimkimbie au nisubiri nione kama kesho atarudia tabia hii.

Asanteni.

Mwambie hata chumbani kwako kuna mashetani, ila wewe unapenda sana ma zombie
 
Kwani ni mamako au dadako? Kama si ndugu yako kinachokufikirisha ni nini? Mpe anachotaka, kwani itakugharimu nini? Au utatakiwa kulipia baada ya kufanya anachotaka ufanye?

kwanza imani yangu hainiruhusu kufanya uzinzi, pili kulikua nauwezekano wa kupoteza malipo yangu yaliobaki after downpayment which i received na mwisho maradhi kwani ingawa namfahamu kwa miaka kadhaa lakini hali yake ki afya sijui.
 
sasa hivi ni alfajiri hapa lakini kwa kweli ni kama sijalala. Alikua akiniamsha bila sababu ya msingi mara oh amka unipigie hesabu tumetumia pesa kiasi gani nikimaliza hata kabla sijalala vizuri naamshwa tena eti nipige simu restaurant watutengenezee chai wakatuletea chai nilipolala tena baadae akaniamsha eti mimi najilalia tu wakati yeye kakosa usingizi yani ananichosha kwa kweli.
 
Mpishe chumba wewe nenda kalale chumba hicho chenye mashetani

alikataa mimi nilale kwenye chumba chake na yeye alale chumbani kwangu. Alidai eti yeye sio chizi kuona mashetani pale kwa hio hata mimi nikilala pale yatakuja tu. Lakini wafanyakazi wa hapa wameniambia kua haijawahi tokea hapa
 
sasa hivi ni alfajiri hapa lakini kwa kweli ni kama sijalala. Alikua akiniamsha bila sababu ya msingi mara oh amka unipigie hesabu tumetumia pesa kiasi gani nikimaliza hata kabla sijalala vizuri naamshwa tena eti nipige simu restaurant watutengenezee chai wakatuletea chai nilipolala tena baadae akaniamsha eti mimi najilalia tu wakati yeye kakosa usingizi yani ananichosha kwa kweli.
hongera kwa kuvishinda vishawishi, akirudia tena VAA CHUPI LA CHUMA
 
Back
Top Bottom