Nirekebishe Vipi tatizo la Blue Screen kwenye Windows 7!?

Nirekebishe Vipi tatizo la Blue Screen kwenye Windows 7!?

Mkuu wa chuo

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2011
Posts
7,626
Reaction score
5,346
Wakuu, nina shida katika Computer yangu kunakuwa na shida tajwa hapo juu kama kunakuwa kunatokea screen ya blue na computer inakuwa inajizima, mara ya kwanza ilikuwa inaingia hadi mwisho.

Ukiwa unapiga kazi mara unashangaa inajizima, zinakuja option kuna ile ya ku repair, na start windows normally, ukichagua hiyo ya kwanza hakuna kitu inarudi hapo hapo, ukichagua hiyo nyingine linatokea tena hiyo shida.

Baadae nikaingia katika safe mode, nikaweka system recovery nikaja kurekebisha nilipo start kawaida ikapiga mzigo kama masaa machache, ikarudia hali hiyo hiyo, kwa sasa mbaya zaidi haingii hata katika safe mode.

Naombeni msaada jinsi ya ku solve hilo tatizo, nina documents sintopenda kuipiga hiyo OS chini, kwasababu nitapoteza, naomba msaada...
 
Wakuu, wataalamu wapo wapi humu, mbona kimya!?
 
Mkuu wa chuo sijaelewa vizuri tatizo lako, Ni Blue Screen Error Au? Hiyo Blue inakuja full Screen si ndio?

Maana kwenye maelezo yako paragraph ya kwanza inaonesha tatizo ni kama Blue Screen, kwenye Paragraph ya pili inaonesha tatizo ni Mashine kujirestart. Au inatoa blue screen halafu inajirestart ?

Nyoosha hapo kwanza ili hata wataalamu wakija wajue pa kuanzia.
 
Mkuu, hiyo blue screen inakuja full screen na maelezo mengi mengi, ni blue screen error... Baada ya muda zinakuja option mbili, ile ya pili inaleta start windows normally, ukiiingia unakuwa kama unazunguka unarudi pale pale kwenye error, kwa sasa inashindwa hata kufika kwenye desktop screen inakuwa inazunguka pale pale...
 
Tatizo linaweza kuwa upande wa software au hardware.

Software:
Kama umeinstall program yoyote hivi karibuni inaweza kuwa ndo inayoleta tatizo, unistall hio program.

Update window ,

Hardware:
Fanya uchunguzi anza kurepair bad sectors kwnye hdd,

Chomoa ram weka ingine uone kama tatizo limeisha.
 
Kuna Tatizo la HDD ambalo huwa linasababisha Blue Screen Lakin kwa maelezo yako inaonesha ni OS Corrupt ya kawaida xo nakushauri ufanye repair au upige window upya. Then Lete feed Back Mkuu wa chuo
 
autorun255,

Jinsi ya ku repair hizo bad sectors unafanyaje!? Hii machine yangu ilivyokaa ni kama zile tv za flat screen halafu ni touch screen pia, cpu na kila kitu zote zipo hapo hapo,nitaweza vipi kufungua na kuchomoa ram!?
 
Last edited by a moderator:
Kuna Tatizo la HDD ambalo huwa linasababisha Blue Screen Lakin kwa maelezo yako inaonesha ni OS Corrupt ya kawaida xo nakushauri ufanye repair au upige window upya. Then Lete feed Back Mkuu wa chuo

Ni tatizo lipi hilo la HDD!? na ni jinsi gani ya kufanya repair ya hiyo OS, nikipiga OS upya si nitapoteza documents zangu!? ambazo ni muhimu... na lengo ni ku save documents...
 
C6 hivi humu hakuna wataalamu wa kuweza kunisaidia hilo tatizo langu !? nisaidie mkuu... tatizo kama hilo nitalitatua vipi!?
 
Mkuu BSOD huwa inasababishwa na tatizo la hardware au software...

Mwenye kuweza kujua haswa chanzo cha tatizo ni wewe mwenyewe kama tu utakuwa makini kufuata steps zifuatazo katika link hii...

Hata tukiandika hapa kuwa tatizo ni kitu fulani bado itakuwa ni ngumu kutoa jibu litalotatua shida hiyo moja kwa moja...

http://m.wikihow.com/Fix-the-Blue-Screen-of-Death-on-Windows
 
Nimeshawahi kupata hili tatizo pia. Hili inaweza kuwa hardware problem kama ulishawahi kuiangusha au ika katika mazingira ya shaking kama kuiweka kwenye boot ya gari.

La pili ni kwamba linatokana na drivers zisizo sahihi kwa laptop/pc yako. Kama umetumia universal drivers au ile software ambayo inainstall all drivers for you. Ningekushauri uende kwenye website ya hiyo laptop/PC yako kisha download proper drivers kisha install.
 
Hiyo Option ya pili unaifanya kwa namna gani!? ikiwa hata kuwaka mpaka mwisho inashindwa!? OS si ndio inaweza ika boot kutoka kwenye cd, lakini hizi software zingine mpaka os ikiwa imetulia ndio unaweza ukafanya...
 
Mkuu BSOD huwa inasababishwa na tatizo la hardware au software...

Mwenye kuweza kujua haswa chanzo cha tatizo ni wewe mwenyewe kama tu utakuwa makini kufuata steps zifuatazo katika link hii...

Hata tukiandika hapa kuwa tatizo ni kitu fulani bado itakuwa ni ngumu kutoa jibu litalotatua shida hiyo moja kwa moja...

3 Ways to Fix the Blue Screen of Death on Windows - wikiHow

Ile option ya ku repair kwa kutumia windows cd ndio naona rahisi... ngojea nicheck hiyo... na hizo zingine nijaribu pia...
 
Back
Top Bottom