Nipsey Hussle afariki kwa shambulio la risasi

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
67,119
173,953
Ni msiba kwa wana hiphop wa kweli hasa kwa wale tunaopenda real stuff. Jamaa ali rep sana mtaa though hakupata airtime kivile.
R.I.P Legend Nipsey Hu$$le

Habari kamili hapo chini, source CNN:

===

Wasanii Drake, Rihanna na J Cole wamlilia rapa Nipsey Hussle, aliyefariki kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo Jumatatu Aprili 1, 2019.

Hussle ambaye jina lake halisi ni Ermias Davidson Asghedom aliuawa nje ya duka lake la nguo huko Los Angeles, Marekani ambako inaelezwa watu wasiojulikana waliokuwa ndani ya gari walimpiga risasi na kufariki wakati akikimbizwa hospitali.

Kifo cha msanii huyo kimewagusa wasanii mbalimbali akiwemo Drake, ambaye aliwania naye tuzo za Grammy za mwaka huu.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Drake aliandika Hussle alikuwa mtu muungwana na mwenye heshima.
Wakati Rihana yeye aliandika waliomfanyia unyama huo ni wapuuzi na kueleza roho yake imetikiswa na tukio hilo ambalo pia limejeruhi watu wengine wawili.

Pia mchezaji mpira wa kikapu maarufu nchini Marekani, Montrezl Harrell, alionyesha hisia za kuguswa na msiba huo kwa kuandika kwenye kiatu chake maneno ya RIP na kuonyesha tarehe na mwaka aliozaliwa na kufariki msanii huyo.
Hussle mwenye umri wa miaka 33, enzi za uhai wake alijizolea umaarufu kupitia nyimbo mbalimbali ikiwemo Bullets Ain't Got No Name series, The Marathon, The Marathon Continues and Crenshaw.

Februari 2018 aliachia albamu aliyoipa jina la Victory Lap iliyofanya vizuri sokoni hadi kumfanya atajwe katika kuwania albamu bora ya rap katika tuzo za Grammy mwaka huu.

Katika kipengele hicho alikuwa akishindanishwa na kina Cardi B, Mac Miller, Pusha T and Travis Scott.
 
Back
Top Bottom