Hiki kisa kimenikumbusha miaka flani ya 2012 nilimtembelea braza Dodoma nilkua napita tu nikaona kwa kua n broza dam dam na miaka ming hatujaonana basi wacha nikite kambi walau kwa siku moja
Sasa kumbe maisha ya bro yamebadilika sana chakula hali tena kama zamani wametenga ka chakula (wali) kwenye ile hot pot ndogo ni kama walipika nusu kilo hivi basi na vipande vya kuku maharagwe kidogo na mboga za majani hahahaha
Ngoja nicheke kidogo





kumbe ndio chakula cha kula familia nzima (bro , mke wake, house girl na mtoto mmoja wa kama miaka sita hvi na mimi mgeni wao) basi wakanikaribisha huku wakinisisitiza nikapakue
Basi mzee nikainuka kwenda mezani nilivoona ule msosi akili ikaniambia kwa jinsi hiki chakula kilivyo kidogo itakua ni changu peke yangu nilipakua ule wali zaid ya robo tatu tia mboga ya majani na maharage na vipande kama vitatu vya kuku
Sasa baada ya dakika chache huku naendelea kuchakata nawaona na wao wanakuja mezani
Ilibidi niulize kwani na nyie ndio mnakula hiki hiki huku nikiwa na mshangao na taharuki ya hali ya juu ikabidi wajichekeshe chekeshe pale house girl akaingia jikon kupika ugali
Kesho yake niliamsha bila hata kupata breakfast maana siwezi kukaa nyumba yenye njaa mimi