Nianze tu kwa kumpongeza Mh rais kwa majukumu mazito na magumu ya kiutendaji katika taifa letu. Pia nimpe pole sana kwa changamoto nzima anazozipata juu ya utekelezaji wa ilani ya chama chake cha mapinduzi (CCM)
Lakini pia nitumie nami nafasi hii kumfikishia ujumbe wangu na ujumbe wa wana Nyamongo kwa ujumla
Mh rais,ulipopita nyamongo mnano 2015,ulisikika ukiwambia wananchi wa nyamongo juu ya kero yao ya mgodi na nao juu ya mambo yafuatayo-:
(a).Fidia ya malipo (compensation)
(b).Maji
Mh Rais,nitajikita zaidi ktk kero ya fidia ambayo ndiyo has a kero inayosumbua kuliko kero zote. Suala la fidia ambalo wew mwenyewe uliagiza lifanyike Hata kabla hujawa rais wa taifa letu halijafanyika,halijatekelezwa na mgodi unasema hakuna wa kuwauliza kwa sababu serikali ipo mfukoni mwao
Mh rais,kwa mjibu wa sheria ya madini No 14 ya 2010 Inatamka wazi kuwa.
Ni marufuku mgodi kuendeshea shughuli zake ndani ya makazi ya watu,wananchi wanatakiwa kuw a Nje ya mita 200.
Lakini hadi naandika waraka huu kwako,wananchi wanaishi ndani ya mita 10.
Mh rais, tunashindwa kuelewa tatizo lipo wapi?
Je ni sheria au wasadizi wako?
Tumekuwa tukilalamika kwa wasaidizi wako Mara kwa Mara lakini hatuoni juhudi zozote zikichukuliwa zaidi ya kukamatwa na polisi na kubandikiwa kesi
Mh rais kama hautajali nitakulipia nauli,chakula,na malazi ufike nyamongo utusaidie
Tarehh 5/7/2017 alipokuja makamo wa rais,alipelekwa sehemu nyingine na hakufika maeneo ya nyamongo mgodini,na Hata aliporudi tena mwezi wa name kwa ajili ya kuweka jiwe LA msingi MTO mara, alipitishwa pembeni na viongozi wako wa wilaya na mkoa walifanya jitihada ili asifike nyamongo mgodini ili ashuhudie watu tunavyoumia
Tumeumizwa sana,Tumechoka sana,tunakuomba MKUU ufike nyamongo utusaidie tupate haki
Tunaamini unasimama ktk haki na haki itatendeka Ukisimama wewe,
Migodi hii unaijua vizuri sana jinsi walivyo wataalamu wa kuhonga na kutoa rushwa
Sisi wananchi wa nyamongo tunakuomba kwa heshima kabisa uje rule kichule kama ulivyotuhaidi wakati ule
Mwisho tunakutakia kazi njema
Kwa niaba ya wananchi wa nyamongo
...............
Mzalendo