Nipo tayari kulipa gharama zote za nauli, chakula na usafiri kwa Rais Magufuli akikubali kuja Nyamongo Tarime, Mara

Jinokali

New Member
Sep 29, 2017
2
45
Nianze tu kwa kumpongeza Mh rais kwa majukumu mazito na magumu ya kiutendaji katika taifa letu. Pia nimpe pole sana kwa changamoto nzima anazozipata juu ya utekelezaji wa ilani ya chama chake cha mapinduzi (CCM)

Lakini pia nitumie nami nafasi hii kumfikishia ujumbe wangu na ujumbe wa wana Nyamongo kwa ujumla
Mh rais,ulipopita nyamongo mnano 2015,ulisikika ukiwambia wananchi wa nyamongo juu ya kero yao ya mgodi na nao juu ya mambo yafuatayo-:

(a).Fidia ya malipo (compensation)
(b).Maji

Mh Rais,nitajikita zaidi ktk kero ya fidia ambayo ndiyo has a kero inayosumbua kuliko kero zote. Suala la fidia ambalo wew mwenyewe uliagiza lifanyike Hata kabla hujawa rais wa taifa letu halijafanyika,halijatekelezwa na mgodi unasema hakuna wa kuwauliza kwa sababu serikali ipo mfukoni mwao

Mh rais,kwa mjibu wa sheria ya madini No 14 ya 2010 Inatamka wazi kuwa.
Ni marufuku mgodi kuendeshea shughuli zake ndani ya makazi ya watu,wananchi wanatakiwa kuw a Nje ya mita 200.

Lakini hadi naandika waraka huu kwako,wananchi wanaishi ndani ya mita 10.

Mh rais, tunashindwa kuelewa tatizo lipo wapi?
Je ni sheria au wasadizi wako?
Tumekuwa tukilalamika kwa wasaidizi wako Mara kwa Mara lakini hatuoni juhudi zozote zikichukuliwa zaidi ya kukamatwa na polisi na kubandikiwa kesi

Mh rais kama hautajali nitakulipia nauli,chakula,na malazi ufike nyamongo utusaidie

Tarehh 5/7/2017 alipokuja makamo wa rais,alipelekwa sehemu nyingine na hakufika maeneo ya nyamongo mgodini,na Hata aliporudi tena mwezi wa name kwa ajili ya kuweka jiwe LA msingi MTO mara, alipitishwa pembeni na viongozi wako wa wilaya na mkoa walifanya jitihada ili asifike nyamongo mgodini ili ashuhudie watu tunavyoumia

Tumeumizwa sana,Tumechoka sana,tunakuomba MKUU ufike nyamongo utusaidie tupate haki

Tunaamini unasimama ktk haki na haki itatendeka Ukisimama wewe,

Migodi hii unaijua vizuri sana jinsi walivyo wataalamu wa kuhonga na kutoa rushwa

Sisi wananchi wa nyamongo tunakuomba kwa heshima kabisa uje rule kichule kama ulivyotuhaidi wakati ule

Mwisho tunakutakia kazi njema
Kwa niaba ya wananchi wa nyamongo
...............
Mzalendo
 
Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,659
2,000
MKUU UNAUJUA UKUBWA WA MSAFARA WA RAISI LAKINI??!!Afu ujue zile ni ahadi tu mkuu na ahadi sikuzote huwa yenye kutekelezeka au kinyume chake [HASHTAG]#2020[/HASHTAG]
 
G4rpolitics

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
3,682
2,000
Nilishamwandikia nyuzi nyingi mkuu za kumlaani kwa nini haji Mara lakini inaobekana siku hizi haingii jf.
 
silent kills

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
568
1,000
MKUU UNAUJUA UKUBWA WA MSAFARA WA RAISI LAKINI??!!Afu ujue zile ni ahadi tu mkuu na ahadi sikuzote huwa yenye kutekelezeka au kinyume chake [HASHTAG]#2020[/HASHTAG]
Alisema zile zilikuwa ndumba za kuombea kura Tu...nyie kama mliamini atakuja basi ashawapa maelezo Kwamba aliyoyasema kipindi cha campaign yalikua maneno matamu ili mumpe kura...ila HAYATEKELEZEKI
 
MAGALLAH R

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
946
1,000
Rais wetu ni msikivu na amekusikia atayafanyia kazi hayo uliyomwambia ondoa shaka na tegemea nyamongo mpya
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
46,978
2,000
MKUU UNAUJUA UKUBWA WA MSAFARA WA RAISI LAKINI??!!Afu ujue zile ni ahadi tu mkuu na ahadi sikuzote huwa yenye kutekelezeka au kinyume chake [HASHTAG]#2020[/HASHTAG]
Andaeee billion moja Kwa ajili ya garama ya matumizi ya mkulu

Ova
 
mjumbe wa bwana

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
4,048
2,000
naamini kuna chama kikitoa ahadi 100 basi 89 zinakuwa nizaongo sasa jichunguze usije kuta ndo hicho chama unakizungumzia. ila vuta subira [HASHTAG]#2020[/HASHTAG] ukafanye kweli
 
iJamii

JF-Expert Member
Jan 19, 2015
1,982
2,000
MKUU UNAUJUA UKUBWA WA MSAFARA WA RAISI LAKINI??!!Afu ujue zile ni ahadi tu mkuu na ahadi sikuzote huwa yenye kutekelezeka au kinyume chake [HASHTAG]#2020[/HASHTAG]
Nnahisi hafahamu ukubwa wa msafara wake unakuwaje au labda mwenzetu ni mmoja kati ya wale ambao nao wanatakiwa kuishi kama mashetani
 
lwamu

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
933
1,000
Bora umsubir Tundu Lissu apone umpe hiyo rai.....kwa maana yeye ndo mpigania haki za wanyonge...#TL_4_PRESIDENTIAL_2020.
 
Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
7,892
2,000
MKUU UNAUJUA UKUBWA WA MSAFARA WA RAISI LAKINI??!!Afu ujue zile ni ahadi tu mkuu na ahadi sikuzote huwa yenye kutekelezeka au kinyume chake [HASHTAG]#2020[/HASHTAG]
Kazoea kumlipia dada wa kazi nauli anadhani ni sawa na rais. Vichwa vingine ni vta kufugia nywele tu.
 
son of a teacher

JF-Expert Member
Jul 30, 2017
365
1,000
Kazoea kumlipia dada wa kazi nauli anadhani ni sawa na rais. Vichwa vingine ni vta kufugia nywele tu.
Wenye IQ kubwa tumemuelewa mtoa thread kamaanisha tokea kipindi cha kampeni na kuahidiwa ahadi kedekede mh rais hajakanyaga tena nyamongo na watu wa nyakongo wana shida zao na wanataka rais wamfikishie

Mfano rais magufuli akisoma thread hii atajisikia haya yani mpaka wanataka wanilipie usafiri kweli hawa wana shida na wananihitaji so hata kama hakuwa na mpango wa kwenda atajisikia aibu na kuratibu mipango ya kwenda
 
kirikou1

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
3,937
2,000
Ili kupunguza gharama bora aende banana au kitunda aonane na wawakilishi wa nyamongo. Teh teh
 
Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
5,266
2,000
Nianze tu kwa kumpongeza Mh rais kwa majukumu mazito na magumu ya kiutendaji katika taifa letu. Pia nimpe pole sana kwa changamoto nzima anazozipata juu ya utekelezaji wa ilani ya chama chake cha mapinduzi (CCM)

Lakini pia nitumie nami nafasi hii kumfikishia ujumbe wangu na ujumbe wa wana Nyamongo kwa ujumla
Mh rais,ulipopita nyamongo mnano 2015,ulisikika ukiwambia wananchi wa nyamongo juu ya kero yao ya mgodi na nao juu ya mambo yafuatayo-:

(a).Fidia ya malipo (compensation)
(b).Maji

Mh Rais,nitajikita zaidi ktk kero ya fidia ambayo ndiyo has a kero inayosumbua kuliko kero zote. Suala la fidia ambalo wew mwenyewe uliagiza lifanyike Hata kabla hujawa rais wa taifa letu halijafanyika,halijatekelezwa na mgodi unasema hakuna wa kuwauliza kwa sababu serikali ipo mfukoni mwao

Mh rais,kwa mjibu wa sheria ya madini No 14 ya 2010 Inatamka wazi kuwa.
Ni marufuku mgodi kuendeshea shughuli zake ndani ya makazi ya watu,wananchi wanatakiwa kuw a Nje ya mita 200.

Lakini hadi naandika waraka huu kwako,wananchi wanaishi ndani ya mita 10.

Mh rais, tunashindwa kuelewa tatizo lipo wapi?
Je ni sheria au wasadizi wako?
Tumekuwa tukilalamika kwa wasaidizi wako Mara kwa Mara lakini hatuoni juhudi zozote zikichukuliwa zaidi ya kukamatwa na polisi na kubandikiwa kesi

Mh rais kama hautajali nitakulipia nauli,chakula,na malazi ufike nyamongo utusaidie

Tarehh 5/7/2017 alipokuja makamo wa rais,alipelekwa sehemu nyingine na hakufika maeneo ya nyamongo mgodini,na Hata aliporudi tena mwezi wa name kwa ajili ya kuweka jiwe LA msingi MTO mara, alipitishwa pembeni na viongozi wako wa wilaya na mkoa walifanya jitihada ili asifike nyamongo mgodini ili ashuhudie watu tunavyoumia

Tumeumizwa sana,Tumechoka sana,tunakuomba MKUU ufike nyamongo utusaidie tupate haki

Tunaamini unasimama ktk haki na haki itatendeka Ukisimama wewe,

Migodi hii unaijua vizuri sana jinsi walivyo wataalamu wa kuhonga na kutoa rushwa

Sisi wananchi wa nyamongo tunakuomba kwa heshima kabisa uje rule kichule kama ulivyotuhaidi wakati ule

Mwisho tunakutakia kazi njema
Kwa niaba ya wananchi wa nyamongo
...............
Mzalendo
You must be Joking kumsafirisha Rais? Je unajua ile kuongea tu na Wananchi analipwa Msafara wake je na kadha wa kadha
 
Mlatinoh king

JF-Expert Member
Oct 14, 2015
5,113
2,000
Hahahahaaaa hii nchi mambo yamekuwa magumu mpka wengine mnaanza kuwa wehu sasa........umesema upo tayar kumfanyia nini Ili aje kwenu????????????
 
Top Bottom