Ushirombo
JF-Expert Member
- Jan 22, 2013
- 3,558
- 2,698
Wakuu nipo songea takribani wiki sasa, kuna mzee maeneo ya bomba mbili katika kudadisi asili ya jina na historia ya songea,akatiririka kwa kadiri ya uelewa na kimbukumbu zake, anasema songea ni jina la mwanaume aliyekua mtemi maeneo haya,katika kurupushani na wajermani watanganyika 66 walikamatwa na yeye mtemi songea akiwemo,waliwekwa gerezan muda mrefu huku kesi yao ikiwa ipo mahakamni huko germany, ilitoka hukumu mwaka 1906 kuwa wanyongwe,except songea,so wale watanganyika akiwemo mwanamke mmoja walinyongwa na kuzikwa kaburi moja, issue ikawa kwa songea wakampa mashart ya kumtoa awe huru ila awe anafanyakaz kwa matakwa ya mjerman coz yeye tayar anasikilizwa na watu na kuheshimika,jamaa akakataa akasema ni bora mniue tu kama wenzangu,siku tati baadae wakamnyonga na yeye akazikwa kaburi lake peke ake, Story hiyo nimeconfirm leo asbh tbc radio.So hapo ndo mji songea ukaitwa jina la huyo shujaa.Kuna kitu cha kujifunza jamani.