Nipo njiapanda

maimatha

Senior Member
Joined
Mar 2, 2013
Posts
129
Reaction score
162
Ninamtoto wa miezi mitatu niliezaa nae aliniambia nitoe nikakataa basi tukawa tumekosana alinifanyia visa vingi nilikua nyumbani nimejingua nikamjulisha aliuliza jinsia tu hakuendelea na mawasiliano kimya mpaka sasa.

Kilichonifanya nije hapa

kuna kaka alikuwa ana mke hawakufunga amezaa nae mtoto mmoja akampeleka chuo huko akazaa tena na mwanaume mwingine wakawa wameachana huyo kijana akamchukua mtoto wake.

Sasa kaja anataka kunioa mimi nimemwambia siwezi mtoto wangu bado mdogo anavyodai kanipenda kweli mtoto wake anateseka alipo ni kwa mama wake wa kambo na huyo kijana so anataka tuishi pamoja.

Upande wangu sasa

1) Sijui kwanini bado nampenda sana baba mtoto nasubiria muujiza wa Mungu labda atarudi na tutaishi pamoja kwani sipendi kuzaa watoto baba tofauti basi tu ishatokea.

2) Nitamwaminije kama yupo serious? isije ikawa ndo yale yale tena maana anadai tuishi pamoja wakati anafanya mipango ya ndoa.

3) Nahisi mtoto bado mdogo angalau angekua anamwaka, sijui niamue nini kwa sasa naombeni tu mnisaidie mawazo nifanye nini ndugu zanguni?
 
unasubiria miugiza babamtoto arudi wakati alikataa kulea mimba... kweli kuna wanawake wanaamini miugiza kwenye mapenzi labda ukaloge dawa ikiisha ufukuzwe we na mwanao... new guy mpe muda yawezekana kweli anakupenda au anataka ukawe yaya wa mwanawe pia... think... lakini muugiza wa uliezaa nae nakuomba usiufikirie utakufa uache mtotto mdogo...
 
kwa kweli ukisubiria muujiza wa huyo aliekana mimba aje tena ni uongo angalia moyo wako ulipoelekea maana mwisho wa siku ni maish yako yapo mikonon mwako. hata siku moja huwez kujua utam wa ngoma kwa kuangalia na macho lazima uingie ucheze mwenyewe.
 
Huyo anayetaka kukuwowa ukiwa na mtoto mchanga amekwisha wahi kukugegeda? Kama bado kimbia haraka,
cha msingi ni kujitafutia njia ya kupata kipato uendeleze maisha wewe na mwanao. Achana na mambo ya mahusiano/ndoa. Ipe muda akili yako itulie, kwa sasa hauko sawa.
 
Iv dunia hii ya sasa kuna miujiza mikubwa namna hio????
 
Mmmmhhh mambo ya mapenzi mimi huwa napata kigugumizi kutoa ushauri. Anyway....mi ushauri wangu ni kwamba achana na fikra za huyo baba wa mtoto wako usijekuwa unasubiria meli ubungo....huyo kijana anayeyaka kukuoa mwambie akusubiri mtoto akue na usishiriki nae mapenzi hadi mtoto aache kunyonya. La mwisho usikubali kuhamia kabla ya ndoa...hakikisha umefunga ndoa ndo uende kwake. Limeshafanyika kosa moja kwa hiyo kuwa na msimamo thabiti usifanye kosa la pili....pliiz usijirahisishe.
 
tusubiri Tyta aje atuhakikishie kasema muongo
 
Last edited by a moderator:
mkuu pole sana kwa matatizo. the problem here is your heart, it wants to get involved in everything in your life rather than doing its most important job i.e pumping blood. first of all achana na mawazo ya huyo baba mtoto wako..[disgrace to we men].

kuhusu huyo mwanaume mpya, kama unampenda[ dont do it out of desperation that you need a man], mwambie mfanye process za ndoa kwanza ndo muishi pamoja.. apart from that i still can smell the same heart breaking story ahead. NDOA KWANZA...

usifanye maamuzi kutokana na matatizo uliyonayo, a happy ending doesnt include a guy,may be its you and your own picking up the pieces and starting over,freeing yourself up for something better in the future.

ALL THE BEST MKUU.
 
Mwambie Akusubir Ulee Mtoto Afikie Miaka 2 Hiv Harafu Akuwowe Kama Kweli Amekupenda Ucimpe Papuchi Mpaka Ufunge Ndoa
 
hivi ndoa ni kitanzi kwa wanandoa kwamba hata kama ndoa inakunyonga uvumilie? cha msingi procedures zote zifuatwe hasa mahari, mtu akifunga ndoa haina maana kuwa hawezi kukuacha au kuoa mke mwingine, ni jinsi maisha, hulka, tabia na mioyo yenu itakavyojielekeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…