Nipo njia panda sijui lipi la kufanya

mzee wa ndoto

Member
Jul 10, 2020
75
46
Habari wanajamii,

Ushauri wenu itakuwa msaada tosha katika hili.

Baba mkwe wangu aliniomba mwanaye (mke wangu) aende akamsaidie kuvuna mpunga nami nikamruhusu. Makubaliano baada ya miezi 2 atarudi ilipofika miezi hiyo baba mkwe kwenye simu hapatikani na mke wangu hapatikani.

Mashamba yao yako Moro vijijini Rondo Mbingu kwake Moro mjini na Mimi ndipo ninapopajua.

Nikakumbuka namba moja mke wangu alipokuwa kule tulishawahi kuongea. Nikapiga ile namba simu ilipopokelewa nikajitambulisha na kumuelekeza jamaa akanielewa na nikamueleza lengo la kumpigia simu kutaka kujua ya mke wangu. Jamaa akanijibu kuwa yeye yuko mbali na yeye yuko Ifakara mjini hivyo baada ya mwezi mmoja ataenda Mbingu ataniunganisha na familia yangu.

Kweli baada ya mwezi mmoja Mimi nilimtafuta jamaa bila mafanikio nikatoa taarifa kwa ndugu wengine wa mke wangu wakajibu nisiwe na hofu yupo kwa baba yake. Kama miezi saba jamaa alinitafuta yeye na kunielezea kuwa alikuwa anaumwa; ilifikia hatua mpaka kuuza simu ndio maana sikuwa nikimpata. Baada ya hapo akaniunganisha na mke wangu yaani nilihisi kama ndoto; tulianza na salamu kwangu ilikuwa furaha lakini kwa mwenzangu ni majibu ya mkato tu.

Nilipo muliza kulikoni kuchelewa kurudi nyumbani na kukosa kunitafuta kwenye simu, majibu hayaelewaki lawama za uongo mwisho nikamwambia natuma nauli leo kesho nataka urudi nyumbani, akanijibu suala la mimi kuludi huko sahau. Kuhusu watoto wakikushinda kulea wahamishe shule Ila mimi sirudi na simu ikakata.

Nilimpigia tena akapokea mwenye simu nikamuuliza yupo akanijibu hapana kaondoka yuko kule na baba yake. Nikamwambia naomba niunganishe naye aliponiunganisha na mzee nikaongea naye salama kisha nikampa lawama za mwanaye kuwa hataki kurudi nyumbani. Baba mkwe alichojibu kuwa mke wako amenogewa na huku hivyo sahau suala kurudi huko.

Jamaa yangu mwenye simu tukawa marafiki, sasa akaniuliza kuhusu mke wangu nilimuoa au tumeokotezana nikamjibu nimeoa. Akaniambia njoo ufumanie, yuko na mtu. Kiukweli niliumia sana nilipopata tarifa hizi ingawa mwenyewe nilikuwa nahisi hivyo pia.

Nakumbuka hiyo ilikuwa mwezi wa tatu mwaka huu na yeye aliondoka mwezi wa tatu mwaka jana. Ilinibidi niungeunge nauli ya kwenda na kurudi yangu na ya mke wangu Dar -- Ifakara_16000 Ifakara-- Rondo 8000 bodaboda 8000. Nami nilienda na laki na nusu.

Tare 26/7/2020 nilifika Rondo jamaa yangu aliniekeza mpaka pale ukweni nikafika mke wangu alitahay sana. Hata Mimi nilipigwa na butwaa nisijue nini cha kufanya baba mkwe kanikimbia mpaka leo bado hajarudi.

Kibaya zaidi, mke wangu ana mimba. Hapa nyumbani yuko yeye na shangazi yake; juzi nilipokuja kuna jamaa alikuwepo Ila toka hiyo juzi sijamuona.

Mzee hayupo; jamaa yangu mda wote ni mtu wa kunipa nasaha tu. Niko njiapanda ata sielewi cha kufanya nimechanganyikiwa.

Ahsante pia pole kwa usumbufu
 
Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wanawake ni kubwa kuliko wanaume! Achana nae huyo wewe lea watoto waje wakusaidie kesho ukiwa mzee! Wenye vitobo ni wengi hapa mjini msahau huyo
 
Duh kwahiyo umekuja kuomba ushauli? Nikikupa ushauri utaupokea au lazima uwe ushauli?

Anyway ngoja nikupe ushauli. Mtie mimba na wewe, mtafute baba mkwe mpe mimba pia, huyo shangazi yake tia mimba pia, huyo jamaa ambaye hujamuona tangu juzi mtafute tia mimba, huyo aliyekuita ufumanie tia mimba na atakayehoji kwanini unatia mimba wenzako na yeye tia mimba.
 
Huna haja ya kupasuka kichwa. Wanawake wengi sana beba mwingine maisha yaendelee, huna haja ya kupoteza muda kwa Malaya
 
Mpelekee watoto awalee ww uwe unatuma matunzo.

Rudi mjini pambana , tafuta mtoto mbichii mzuri zaid yake kula mema ya nchi.

Na this time usioe, we vuta ndan jilie vyako.

Na ni Aibu kwake wala sio kwako, so usijishtukie kwamba mke kakukimbia
 
Ok nimesoma hii stori yako,sasa huyo mkeo mlifunga ndoa wapi?,kule mlikofungia ndio peleka malalamiko yako ili mgogoro huo upatiwe ufumbuzi
 
Pole sana dingi,
Hapo anza maisha yako upya,lea watoto au mpelekee utume matumizi
Wewe na yeye sahau.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom