Nipo njia panda kijana mwenzenu..

Nipo njia panda kijana mwenzenu..

Habari zenu wana jamvi wenzangu? Mimi nina boyfriend ambaye tumekuwa kwenye mahusiano karibia mwaka wa tano sasa. Kinachoniweka njia panda ni kwamba tunapendana sana lakini mama na ndugu wengine hawataki tuoane kwasababu kwanza makabila tofauti, wanataka niolewe na mtu wa kabila langu, kingine kielimu nimemzidi na nyumbani wanataka at least tuwe level moja au aliyenizidi elimu, halafu mwanaume ni mfupi mimi ni mrefu tukipita njiani watu wanajua yupo na dada yake kumbe ni girl friend wake. Naomba mnishauri nifanyeje kwa sababu kumpenda nampenda, nikimuacha nitamuumiza na sitaki kumuumiza na mama yangu naye nampenda sitaki kumuumiza, nifanyeje?

Umesema ukimuacha utamuumiza, vipi kuhusu upande wako,hautaumia? kosa kubwa mtu analoweza kulifanya ni kuwa na mtu kwasababu ya kumuonea huruma. Kwa namna ninavyoona ni kwamba taratibu unaanza kukubaliana na hayo yanayosemwa, hasa unapotilia mkazo kuwa "halafu mwanaume ni mfupi mimi ni mrefu tukipita njiani watu wanajua yupo na dada yake kumbe ni girl friend wake " hata kama ni ukweli namna unavyosema inaonekana kwamba hata wewe imeanza kukukera. Cha msingi tafakari juu ya nini unachokitaka,fanya maamuzi yako bila kuwa influenced na mtu mwingine yeyote, na kama some of previous comments sinavyosema, unaweza kupata mtu mwenye vigezo vyote vya nje lakini mwishowe ukaja kujuta. Wazazi wanaweza yaliyomema kwa wanawe lakini since nao ni humans kuna muda wanakosea pia. Taratibu wataelewa hasa wakiona upendo wenu ni wa kweli na kwamba utakua salama kwenye mikono yake.
Problems zipo kwenye every relationship but its you to decide whether they are a stumbling block or stepping stone to your happy ending.
Kubwa zaidi ya yote ni maombi, ambalo haliwezekani machoni petu kwa MUNGU yanawezekana. Best of Luck
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom