Pretty R.
JF-Expert Member
- Apr 14, 2012
- 200
- 31
Habari zenu wana jamvi wenzangu? Mimi nina boyfriend ambaye tumekuwa kwenye mahusiano karibia mwaka wa tano sasa. Kinachoniweka njia panda ni kwamba tunapendana sana lakini mama na ndugu wengine hawataki tuoane kwasababu kwanza makabila tofauti, wanataka niolewe na mtu wa kabila langu, kingine kielimu nimemzidi na nyumbani wanataka at least tuwe level moja au aliyenizidi elimu, halafu mwanaume ni mfupi mimi ni mrefu tukipita njiani watu wanajua yupo na dada yake kumbe ni girl friend wake. Naomba mnishauri nifanyeje kwa sababu kumpenda nampenda, nikimuacha nitamuumiza na sitaki kumuumiza na mama yangu naye nampenda sitaki kumuumiza, nifanyeje?