Nipo natizama TBC nashangaa!

Nipo natizama TBC nashangaa!

Craig

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2013
Posts
1,676
Reaction score
3,139
Wanajamvi heri ya sikukuu ya Nyerere Day,

Nipo nyumbani naangalia TBC naona tangazo la Magufuli anaomba kura. Nikakumbuka wakati kampeni zinaanza kuna bango la Lowassa lilitolewa pale sokoni Kariakoo kwa madai kuwa soko ni mali ya umma kwa hiyo halifungamani na upande wowote kwa mantiki hiyo hakuna ruhusa ya kuweka mabango ya kisiasa kwene soko hilo.

Sasa leo naona tangazo la Magufuli TBC akiomba kura. Najiuliza hii TBC si ni mali ya umma pia. Inawezaje kujihusisha na matangazo ya kisiasa, ikiwa inaendeshwa kwa kodi za wananchi na siyo kibiashara. Je, tofauti ya TBC na shirika la masoko la Kariakoo katika umilikiwaji wake nini?

Nawakilisha.
 
CCM hawafai kuiongoza nchi hii.WAooo ndio wezi na wavunja sheria wakuu
 
Pengine amelipia tusitangaze sana chuki kama hatuna uhakika
 
Wanajamvi heri ya sikukuu ya Nyerere Day,

Nipo nyumbani naangalia TBC naona tangazo la Magufuli anaomba kura. Nikakumbuka wakati kampeni zinaanza kuna bango la Lowassa lilitolewa pale sokoni Kariakoo kwa madai kuwa soko ni mali ya umma kwa hiyo halifungamani na upande wowote kwa mantiki hiyo hakuna ruhusa ya kuweka mabango ya kisiasa kwene soko hilo.

Sasa leo naona tangazo la Magufuli TBC akiomba kura. Najiuliza hii TBC si ni mali ya umma pia. Inawezaje kujihusisha na matangazo ya kisiasa, ikiwa inaendeshwa kwa kodi za wananchi na siyo kibiashara. Je, tofauti ya TBC na shirika la masoko la Kariakoo katika umilikiwaji wake nini?

Nawakilisha.

Inasikitisha sana kama upeo wa wana mageuzi ndiyo huu wa kulalamika tu kama wake wenza bila hata kufikirisha akili kidgo, basi ccm itaongoza nchi hii kwa muda mrefu sana. Jitahidi kuangalia TV zote usisuse kama mtu aliyekata tamaa then utapata jibu
 
TBC imekaa kimaslahi ya chama tawala. Nakumbuka mwaka 2010 chini ya Tirdo Mhando, wagombea wa chama tawala walikatazwa kushiriki na kisha kupelekea kufungiwa kwa kipindi cha "mchakato majimboni" kwakuwa kipindi hicho kilionesha madudu ya wagombea wa chama tawala.

Haikuishia hapo. Tirdo mwenyewe kibarua kikaota majani!

Nina miaka minne sjaangalia chochote TBC! Hata kombe la dunia nlikataa kuliangalizia TBC!
 
Wewe kama huoni tofauti kati ya TVT na soko you are beyond repair

Wanajamvi heri ya sikukuu ya Nyerere Day,

Nipo nyumbani naangalia TBC naona tangazo la Magufuli anaomba kura. Nikakumbuka wakati kampeni zinaanza kuna bango la Lowassa lilitolewa pale sokoni Kariakoo kwa madai kuwa soko ni mali ya umma kwa hiyo halifungamani na upande wowote kwa mantiki hiyo hakuna ruhusa ya kuweka mabango ya kisiasa kwene soko hilo.

Sasa leo naona tangazo la Magufuli TBC akiomba kura. Najiuliza hii TBC si ni mali ya umma pia. Inawezaje kujihusisha na matangazo ya kisiasa, ikiwa inaendeshwa kwa kodi za wananchi na siyo kibiashara. Je, tofauti ya TBC na shirika la masoko la Kariakoo katika umilikiwaji wake nini?

Nawakilisha.
 
Ndo maana tunataka iondolewe. Hawazi kutenganisha chama na serekali. Kwa wao ni kutu kimoja. Sasa wakika benchi watajua kumbe zile mali zilikua za uma na sio za ccm, watanyoka.
Chama kinanufaika sana inavyooneka na fedha na mali za uma. Ni aibu sana ku hodhi mali ya uma na kuyafanya yao. Ndo maana tuna sema mfumo wa ccm mmbaya sana na tumeuochoka waende zao hawa jamaa. Wametutia hasara sana kwenye hii nchi.Mashirika ya uma yapo taabani bin taabani kwa sababu ya wao. Hii ndo dozi yao mwaka huu, na wataondoka kiulaini sana.
 
Wanajamvi heri ya sikukuu ya Nyerere Day,

Nipo nyumbani naangalia TBC naona tangazo la Magufuli anaomba kura. Nikakumbuka wakati kampeni zinaanza kuna bango la Lowassa lilitolewa pale sokoni Kariakoo kwa madai kuwa soko ni mali ya umma kwa hiyo halifungamani na upande wowote kwa mantiki hiyo hakuna ruhusa ya kuweka mabango ya kisiasa kwene soko hilo.

Sasa leo naona tangazo la Magufuli TBC akiomba kura. Najiuliza hii TBC si ni mali ya umma pia. Inawezaje kujihusisha na matangazo ya kisiasa, ikiwa inaendeshwa kwa kodi za wananchi na siyo kibiashara. Je, tofauti ya TBC na shirika la masoko la Kariakoo katika umilikiwaji wake nini?

Nawakilisha.

Achana na TBC.

Huo muda unaotumia kuangalia TBC bora ukawaogeshe wanao au kucheza na mke wako.
 
Usijidanganye. Baada ya Chadema kununuliwa na Lowassa (kwa bei ya jumla) mwisho bado uko mbali sana.

Huyu Lowassa ana pesa gani kununua kila mtu !!tuliambiwa kanunua watu wanaokwenda kwenye mikutano yake sasa kanunua chama!!.Ccm bring back our Twigas and Tembos.Ccm Out
 
Hivi nyie ukawa c mlishakubaliana humu msiwe mnaangalia tbc wala star tv?asa imekuaje tena mmepatwa na kisabengo cha kuangalia tbc yetu?
 
Back
Top Bottom