Nipeni ushauri wenu tafadhali ananiumiza huyu mwanadada

Nipeni ushauri wenu tafadhali ananiumiza huyu mwanadada

Wadau, naomba ushauri wenu nduguzanguni. Kuna mwanadada mmoja ambaye kwa sasa aliolewa lakini tatizo lake huwa kila mara ananielezea shida za bwanake,anaweza niambia bwanangu jana alilewa na akakosa chakula nipe ksh.100 nikale nina njaa. Wakati mwengine bwanake akiondoka kuenda kazini huwa anakuja nyumbani mwangu huku amevaa minisketi na top pekeyake na akiniona huwa ananivunjia macho,na kutabasamu. Halafu mimi bado sijaoa. Sasa nashindwa sijui nifanyeje ili asinizoe mara kwa mara kwani sitaki kufanya maasi. Na bwanake akijua kuwa anamazoea na mimi ataniletea shida. Nipeni ushauri wenu wana Jf.

Wewe mkunze tu ila muwewe akijua utajua kuwa mke wa mtu ni sumu kali sana. Halafu kuvunjia macho ndiyo kitu gani? Nimecheka sana, sema anakurembulia bwana, yaani ile kulegeza macho kimahaba.
 
Inategemea na utokako, ka ni kenya kwa hiyo alama ya ksh siwezi kusema sana ila humu Tanzania husani kule mara andaa eneo la mazishi yako, ka ni sehemu za kiganga zaidi jua baada ya kuingia mtanatana mpaka ufe na aibu ndo ujue mke wa mtu sumu ila kwa baadhi ya maeneo poa tu we endelea unakula mke wake akijua anakula dada ako na mama yako ili kulinda heshima. OA NA UKAE NA MKEO ACHA MAZOEA NA WAKE ZA WATU HASA WAUME WAKIWA KAZINI

Huu ushauri,umenitia woga hata mimi kwani asije mke wangu anyemelewe nikiwa kazini.
 
Mpaka sasa ushafanya maasi kichwani mwako, malizia tu praktiko mkuu!
 
ksh 100, sio tsh 100 nyie ndio wale mnaofeli ookh.! Mtihani ulikuwa rahisi kumbe ulikuwa na mitego.. Soma neno to neno.

mkuu acha kukurupuka. Ksh. 100 ni sawa na Tsh ngapi? na ukipata jibu hiyo itamtosha kufanyia nini?
 
Mwambie hali halisi akiwa hakuelewi mtishie utamwambia jamaa yake
 
Mwambie hufurahishwi na tabia yake.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom