Wadau, naomba ushauri wenu nduguzanguni. Kuna mwanadada mmoja ambaye kwa sasa aliolewa lakini tatizo lake huwa kila mara ananielezea shida za bwanake,anaweza niambia bwanangu jana alilewa na akakosa chakula nipe ksh.100 nikale nina njaa. Wakati mwengine bwanake akiondoka kuenda kazini huwa anakuja nyumbani mwangu huku amevaa minisketi na top pekeyake na akiniona huwa ananivunjia macho,na kutabasamu. Halafu mimi bado sijaoa. Sasa nashindwa sijui nifanyeje ili asinizoe mara kwa mara kwani sitaki kufanya maasi. Na bwanake akijua kuwa anamazoea na mimi ataniletea shida. Nipeni ushauri wenu wana Jf.