Nipeni sababu 3 za msingi za kutufanya tuamini Magufuli anastahili kuombewa

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,325
152,136
Hivi nini ambacho raisi huyu amekifanya cha kukufanya uamini kuwa amechukua maamuzi mazito na magumu yanayoweza kuhatarisha usalama wake kiasi kwamba sisi wananchi tumuombee.

Je, ni haya?
1.Kubomoa nyumba za masikini?
2.Kufukuza/kusimamisha watumishi wa umma?
3.Kuwapa grace period wafanyabiashara wakubwa wasiolipa kodi?
4.Kutuoa kauli kali kwa Mawaziri,Makatibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa?

Jamani nisaidieni labda kuna ambayo kaagiza/kayafanya ambayo pengine mimi mwenzuni siyajui kama vile;
1.Kukamata na kufungulia mashitaka wanasiasa wakubwa(vigogo) kwa matumiza mabaya ya madaraka.
2.Kuzuia maslahi ya vigogo
3.Kutishia maslahi ya mataifa makubwa yaliyowekeza hapa nchi kama vile kuagiza kupitia upya mikataba yao na serikali au kuisitisha mikataba hiyo
4.Kuagiza mikataba hiyo ipelekwe bungeni mara moja
5.Kuondoa kinga ya raisi kutoshitakiwa
6.kuagiza uchunguzi mpya juu ya kashifa za Escrow, Kagoda, EPA, Meremeta, n.k.

Mwenezuni sielewi labda kaagiza na haya yafanyiwe kazi ndio maana anaomba tumuombee kwa mungu.
 
Kwamikakati aliyoweka ya kuhakikisha matajiri wanalipa kodi stahili,watoto wanasoma bure,njaa inakomeshwa,afya inaboreshwa,mafisadi yanadhibitiwa,uongozi wa uwajibikaji nk tumwombee tuu aweze kutimiza haya na mengine said.
Kwani nani mwingine anaweza kusukuma haya ili naye tumwombee asikengeuke?? Lowasa au mbowe?
 
Kwa Mungu unaenda kuomba ukiwa na HOJA Zenye nguvu.

Kama umeainisha udhaifu wa Rais basi ombea hizo WEAKNESS ziwe STRENGTH ili taifa lipone, maana hakuna Plan B hadi 2020, na Mungu anaheshimu Sheria na Taratibu za kupata haki tunazowekeana.

Usiingie kwenye chumba cha sala ukiwa na chuki za kiukawa wala kiccm.
 
Kwamikakati aliyoweka ya kuhakikisha matajiri wanalipa kodi stahili,watoto wanasoma bure,njaa inakomeshwa,afya inaboreshwa,mafisadi yanadhibitiwa,uongozi wa uwajibikaji nk tumwombee tuu aweze kutimiza haya na mengine said.
Kwani nani mwingine anaweza kusukuma haya ili naye tumwombee asikengeuke?? Lowasa au mbowe?
Wakuombewa walikuwa kina Sokoine lakini siyo hawa wa leo.
 
Kwani kazi ya maombi ni nin?aliyekamili hastahili maombi bali aliye dhaifu, kwa udhaifu uliomuona nao Magufuli ndio sababu hasa ya kukulazimisha wewe umuombee ili akamilike.
 
Hivi nini ambacho raisi huyu amekifanya cha kukufanya uamini kuwa amechukua maamuzi mazito na magumu yanayoweza kuhatarisha usalama wake kiasi kwamba sisi wananchi tumuombee.

Je, ni haya?
1.Kubomoa nyumba za masikini?
2.Kufukuza/kusimamisha watumishi wa umma?
3.Kuwapa grace period wafanyabiashara wakubwa wasiolipa kodi?
4.Kutuoa kauli kali kwa Mawaziri,Makatibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa?

Jamani nisaidieni labda kuna ambayo kaagiza/kayafanya ambayo pengine mimi mwenzuni siyajui kama vile;
1.Kukamata na kufungulia mashitaka wanasiasa wakubwa(vigogo) kwa matumiza mabaya ya madaraka.
2.Kuzuia maslahi ya vigogo
3.Kutishia maslahi ya mataifa makubwa yaliyowekeza hapa nchi kama vile kuagiza kupitia upya mikataba yao na serikali au kuisitisha mikataba hiyo
4.Kuagiza mikataba hiyo ipelekwe bungeni mara moja
5.Kuondoa kinga ya raisi kutoshitakiwa
6.kuagiza uchunguzi mpya juu ya kashifa za Escrow, Kagoda, EPA, Meremeta, n.k.

Mwenezuni sielewi labda kaagiza na haya yafanyiwe kazi ndio maana anaomba tumuombee kwa mungu.[/QUOTE

Muombee afanye hayo unayotaka... . ingekuwa ameshafanya asingesema tumuombee so muombee tu hayo unayoyataka yatatekelezwa.. Pia muombee tu maana yaonekana ni adui yako Na Mungu ameagza muombee adui yako aishi miaka Ming..... Kwahyo ndugu huna budi kumuombea tu
 
Tunastahili kumwombea kwanza ili aachane na kukumbatia ccm kisa tu imemweka madarakani! Kinachoendelea Zanzibar anaijua ila kwa vile ni ccm anaona sawa kupeleka jeshi
 
Back
Top Bottom