ENANTIOMER
JF-Expert Member
- Sep 22, 2014
- 1,419
- 804
Kuna vyama vingi vya walimu kama vile CWT, CHAKAWATA, n.k. Kila siku nasikia vilio vya walimu wengi kuhusu kutosaidiwa na vyama vyao wakati wa shida. Mpaka sasa nahisi vyama vyote ni majanga, hivyo kama kusingekua na sheria ya kunibana nijiunge angalau na chama kimoja cha wafanyakazi, basi mimi nisingejiunga na chama chochote cha wafanyakazi.
Kwa kuangalia penye unafuu, nahitaji kufahamu haya:
Kwa kuangalia penye unafuu, nahitaji kufahamu haya:
- Chama chenye makato kidogo. logic yangu hapa ni kwamba kwakua vyama vyote havina msaada kwa 'member' wake, ni bora nijiunge ktk chama chenye makato kidogo.
- Chama ambacho angalau japo kiongouongo kiko karibu na wanachama wake hasa ktk kuwatatulia matatatizo yao. hapa najua vyote ni majanga, ila kipi angalau.
- Mengine ongezeeni kwa faida ya walimu wapya wanaohitaji kufahamu kuhusu hili swala.