UGONVIMWIKO
Member
- Jan 23, 2012
- 7
- 6
Mheshimiwa mmoja alienda Kijiji cha Lubeho kuomba kura wananchi wakamuwekea Meza ili asimame juu na kumwaga Sera zake,bahati mbaya aliongea mambo mengi sana na kwa muda mrefu sana hadi wananchi wakaboreka na kuanza kuondoka mmoja baada ya mwingine.Kufumba na kufumbua watu wote wakawa wameisha isipokuwa mtu mmoja tu alibaki huku akiwa anamuangalia Mwanasiasa na anatoa Machozi.Yule mwanasihasa akachukia sana watu kuingia Mitini lkn akampenda yule mmoja aliyebaki,akamwambia "Wewe ni mfuasi mzuri sana wa chama chetu maana wenzako wote wameondoka lkn wewe bado upo! Nini kimekukuna ktk hotuba yangu hadi unalia na huondoki? Yule Mwanakijiji akamjibu "Hiyo Meza uliyosimamia ni yangu nasubiri ushuke niipeleke nyumbani!"