Nipe ratiba ya mstaafu aliyekaribu nawe

Nipe ratiba ya mstaafu aliyekaribu nawe

Siwezi kustaafu mpaka mwili ugome kutembea na kufanya kazi
Kazi ina raha yake asikuambie mtu
Sio kwamba sitaki kustaafu kwa sababu sina hela hapana bali kazi ni Ibada kwangu na ni mazoezi tosha
Naenda holidays mara 2 au 3 kwa mwaka
Naendesha baiskeli na pia kutembea
Hela ya pension ikiingia ni akiba na baada ya kustaafu ukifanya kazi hakuna makato ya kodi tena zote zangu
 
Kustaafu kwa TZ ni kama suspention usipokuwa makini.

Iko hivii: kitendo cha kukabidhi ofisi mstaafu hutengwa mazima na mazingira uliyoyazoea na kukulia kwa miaka nenda rudi.

Unapopata ajira ukiwa kijana mdogo, let say 20-25 na kustaafu ukiwa na 60, maana yake miaka uliyoishi kazini ni kipindi kirefu sana kuliko vipindi vingine maishani mwako ulivyoishi kabla na vilivyobaki utakavyoweza kuishi mbeleni, hivyo ofisi ni zimwi litakalobakia kichwani mwako kwa maisha yote yaliyosalia.
.
Hili badiliko la maisha kwa mstaafu lapaswa kutunishiwa misuli namna ya kulipokea ili kulikubali kwa ajili ya afya ya mwili na akili,(wengi hapa ndipo wanapofeli).

Tatizo la binadamu la kulewa sifa pamoja na adabu za bandia kwa ajili ya madaraka wanazopewa ofisini hudhania kuwa ni stahili ya maisha yao yote, na hiki ndicho kiini cha mzizi wa fitina kwa wastaafu waliowengi, kwa kuwa wanapostaafu huvikosa.

Mtu anapostaafu kwa umri mkubwa hujikuta kapoteza mambo mengi yaliyokuwa yakimpa furaha, faraja na ari katika maisha yake ya kila siku: ambapo watoto wake tayari watakuwa walishakua na kujitegemea, kwa sasa hatakuwa na mtoto nyumbani kwake.

Mke aliyemuoa akiwa msichana, sasa anaitwa ni bibi mtu ana wajukuu, hapelekeshwi ovyo na anastahili utulivu kama wa mstaafu mwenyewe.

Aliyoyazoea ya kazini, kuamka mapema, akifika kazini anaheshimiwa na kunyenyekewa, vyote hivyo 'kwaheri'.

Michongo ya ofisini na marupurupu, simu za madaraka hapigiwi na havimstahili tena.

Haya sasa yupo nyumbani kwake bila ya kazi yoyote wadhani maisha yatasonga?

Kabla ya miaka mitano ya kustaafu kwake, yampasa achague kazi mbadala utakazozifanya baada ya kustaafu na azipractise ili kuzizoea mapema.

Kama ni kilimo ama biashara ndogo ndogo azizoee kiukweli ndiyo zitakazomfanya aishi, si kwa ajili ya kipato bali ni kwa sababu ya mpangilio wa ratiba za kazi hizo kuzifanya.

Asipange mambo makubwa ya maendeleo ya kustaajabisha kichwani mwake atakayoyapata kwenye ustaafu, mawazo ya aina hii hupelekea wastaafu wengi kukwama na kutapeliwa., afanya miradi midogo midogo inayoweza kukua.

Kwa hiyo ratiba zake za kila siku zifuate mipamgilio ya miradi yake aliyojianzishia.

Kama ni duka, aamke mapema kulifungua na achelewe kulifunga, ikiwezekana duka hili liwe ni la nyumbani kwake ili kuepuka kusongamana mabarabarani kila uchao.

kama ni mifugo, aamke mapema kuihudumia, kama ni shamba ama bustani ni hivyo hivyo.

Akitoka huko kama ni shamba ama kwenye mazizi ya mifugo, apate kifungua kinywa na kupumzika.

Asipende kula sana mavyakula matamu matamu kwa ajili ya ulinzi wa afya yake, inaeleweka wazi namna umri unavyosonga ndivyo kinga za mwili zinavyopungua na magonjwa nyemelezi yasiyoambukiza yasababishwayo na lishe huweza kuibuka uzeeni.

Mambo mengine sasa ni hoby na kipaumbele cha mtu atavyopenda kuishi.

Hiyo summary nimeelezea maisha yangu ninayoishi baada ya kustaafu miaka kadhaa iliyopita.
nondo maridhawa sana hizi. ni darsa tosha. inaelekea una madini mengi sana rohoni ungeandika kitabu mzee wangu.
ubarikiwe sana mkuu Sakasaka Mao
 
Fuga mifugo soma vitabu vya hiyo mifugo then ratiba utaipa humo humo ukiwa una hangaika nayo
 
daah navoonaga hawa watu wa maofisini tena wengine viongozi wakubwa wa serikali wanavyopauka na kunyata muda mfupi baada ya kuachia ofisi uwa inanipa tafakuri nyingi sana.

unakuta mtu alikuwa sijui mkuu wa wilaya flani, mkurugenzi, rpc au mkuu wa mkoa fulani unamuona adi unatamani wew ndo ujifiche uvunguni
 
Ndio ni ratiba ya siku nzima kutoka mawio hadi machweo. Nataka kujifunza kitu.

Pia kama mstaafu ni wewe mwenyewe sio mbaya ukashare pia.

Sharing is caring.
Nikikaribia kustaf nitao kabinti kadogo ili kalete amshaamsha kwenye familia.
then ratiba zitakuwa kama kawaida ila sasa bi mdogo awe tayari kuishi kijijini ili tufuge na kulima
sitaishi mjini
 
Ndio ni ratiba ya siku nzima kutoka mawio hadi machweo. Nataka kujifunza kitu.

Pia kama mstaafu ni wewe mwenyewe sio mbaya ukashare pia.

Sharing is caring.
Nashauri Moderator wafungue uzi special wa wastaafu ili washee na kubadilishana uzoefu, maana ni janga la kitaifa kwa sasa, wengi wanakufa na kuchanganyikiwa na kikokotoo
 
Mimi ya baba mkwe wangu hata siandiki sana ngoja nicheke chini ya shuka ratiba yake nitaitoa siku nyingine.
 
Ndio ni ratiba ya siku nzima kutoka mawio hadi machweo. Nataka kujifunza kitu.

Pia kama mstaafu ni wewe mwenyewe sio mbaya ukashare pia.

Sharing is caring.
Mstaafu baba angu yupo hapa kapigika balaa na mimi mtoto wake mambo magumu nataman hata nimsaidie ila napambana ......Mungu aanisaidie ili nimsaidie huyu mzeee
 
Mstaafu baba angu yupo hapa kapigika balaa na mimi mtoto wake mambo magumu nataman hata nimsaidie ila napambana ......Mungu aanisaidie ili nimsaidie huyu mzeee
Kwanini usimuombee tu pumziko la milele? Mi signage sababu ya kupambania maisha after retirement!
 
Back
Top Bottom