Nipe ratiba ya mstaafu aliyekaribu nawe

Nipe ratiba ya mstaafu aliyekaribu nawe

Naamka saa kumi na mbili asubuhi, naangalia eneo langu lote kama kuna kilichojiri.
Nawasiliana na muumba wangu kwa kutafakari siku iliyopita na kushukuru au kuomba msamaha pale nilipokengeuka.
Nafanya mazoezi mepesi kisha usafi wa kinywa na mwili. Ratiba hii inafuatiwa na kufungua kinywa kwa chai ya moto.
Saa moja na nusu naingia ofisini ambapo napiga kazi hadi saa kumi na mbili juu ya alama.
Baada ya kufunga ofisi nafunga mahesabu na kupata Dinner, naingia mitandaoni kuperuzi matukio hadi saa nne usiku, ambapo nafanya usafi wa mwili na kujiandaa kulala.
Ratiba yangu iko hivyo miaka yote kwa 24/7/365 na sitegemei kuibadirisha. [emoji23]
safi kiongozi[emoji120]
 
OK inshallah.

Katika kuelekea kustaafu tunabidi tuangalie Umri na mwili na akili , umri wa bindamu yeyote lazima uende mbele na mwili wake huwa unazeeka Ila AKILI huwa haizeeki ila inakua.

Hivyo ili binadamu atoe matokeo yoyote yale hutegemea AKILI na sio mwili au umri , hivyo unapostaafu , unakuwa haujapungukiwa kitu chochote katika swala la kutoa matokeo maana binadamu anaishi kwa kutegemea AKILI zaidi .

Ukilijua hili jambo utaona kuwa kustaafu kazi ukiyokuwa umeajiriwa haimaniishi hauwezi kuendelea kufanya kazi ya kutoa matokeo uwezo unao kuzidi hata vijana wadogo.

Pia Kama unavyojua binadamu ili aishi anahitaji changamoto ili aendelee kuwa active hii ndo maana unawaona watu Kama kikwete ,kinana bado wanafanya au biden Rais wa USA , sio kwamba wana tamaa Ila wanakaa katika changamoto ilk kupata uhai na akili kuwa active.

Hivyo usitoke katika mwendo haijalishi Una umri mkubwa kiasi gani ,maisha yenyewe huwa yana kuruhusu upumzike (Resting) Ila sio kuacha (Quitting)

Unaweza kuona hapo sababu inayowafanya wastaafu kufa mapema , ni kuamua kutoka katika motion na kuzikimbia changamoto.

Maisha hayana kuzeeka wala kustaafu maana maisha hutegemea akili na akili huwa haizeeki hivyo kaa ktk motion utaishi vizuri Sana.
advice safi mkuu. inaelekea kwa wasio na miradi maisha ya kustaafu ni kimbembe sana au?
 
Kama mdau alivyotangulia kusema hapo juu na mimi naongezea kidogo. Kabla ya kustaafu hakikisha una eneo angalau eka moja haijalishi ni mjini au nje ya mji. Jifunze ufagaji kuku hasa wa kienyeji ambao ufagaji wake hauna "stress" na pia jifunze kilimo cha bustani za mboga. Ukilipangilia hilo eneo vizuri linatosha kukupa faida zifuatazo:-
1. Utawauzia majirani zako mayai na kuku utapata pesa.
2. Wewe mwenyewe utatumia kuku na mayai kama chakula
3. Utawauzia majirani zako mboga za majani utapata pesa.
4. Kwa kuwa umri utakuwa umenda sana na mwili unahitaji sana mboga za majani wewe utazipata kwa urahisi.
5. Wakati wastaafu wenzako wanahangaika kutafuta unga na mboga wewe utakuwa unanunua unga/mchele mboga zipo bustanini.
6. Mwili wako utakuwa unaupa mazozezi kwa kulima bustani na kuhudumia mifugo.
7. Ubongo utakuwa unachangamka kila siku kwa kubishana bei na wateja, mifugo inapopata changamoto kama maradhi, mboga zinaposhambuliwa na wadudu n.k.

Kwa wale wenye ujuzi wa ufundi hakikisha unakuwa na kijiwe cha ufundi au upo chini ya mtu mwenye kandarasi za mara kwa mara ili uwe unapiga deiwaka. Kitendo cha kuendelea kufanya kazi kinaupa mwili nguvu ya kuendelea kuishi kwa miaka mingi Kuna mzee namfahamu alikuwa fundi akastaafu 1984 akaendelea na deiwaka zake za ufundi huwezi amini amekuja kushindwa kutembea mwaka juzi tu hapa. Mafundi wenzake wote aliostaafu nao wameshatangulia mbele za haki wengine miezi michache tu baada ya kustaafu. Wengi kilichowaondoa ilikuwa ni unywaji wa pombe na kuachana na kazi ya ufundi na kuamua kukaa kula mafao na kuridhika na pesa walizokuwa wakitumiwa na watoto wao. Sasa hivi huyo mzee akitoka nje anatumia wheelchair lakini hana maradhi yoyote yanayotishia maisha yake isipokuwa tu presha ya kawaida ambayo anameza dawa kila siku na yupo poa kabisa. Na bado kumbu kumbu zake sio mbaya japo kidogo sasa hivi zinaanza kupunguwa.
 
advice safi mkuu. inaelekea kwa wasio na miradi maisha ya kustaafu ni kimbembe sana au?

Hamna unaweza usiwe na mradi Ila ukawa unaendelea kufanya kazi zako binafsi kwa kutegemea aina ya field yako .

Mfano Mimi mzee wangu hana Mardi Ila anafanya kazi katika kampuni .

Maisha ya kustaafu hayana ugumu wowote Ila ugumu hutokea pale unapokuwa idle ndipo MTU hujikuta anakuwa yupo bored.

Lengo langu nimetoa kama alert kuwa ujitahidi uwe na kitu cha kufanya chochote kitkacho Ku-keep busy na kukuingizia pesa.
 
Kama mdau alivyotangulia kusema hapo juu na mimi naongezea kidogo. Kabla ya kustaafu hakikisha una eneo angalau eka moja haijalishi ni mjini au nje ya mji. Jifunze ufagaji kuku hasa wa kienyeji ambao ufagaji wake hauna "stress" na pia jifunze kilimo cha bustani za mboga. Ukilipangilia hilo eneo vizuri linatosha kukupa faida zifuatazo:-
1. Utawauzia majirani zako mayai na kuku utapata pesa.
2. Wewe mwenyewe utatumia kuku na mayai kama chakula
3. Utawauzia majirani zako mboga za majani utapata pesa.
4. Kwa kuwa umri utakuwa umenda sana na mwili unahitaji sana mboga za majani wewe utazipata kwa urahisi.
5. Wakati wastaafu wenzako wanahangaika kutafuta unga na mboga wewe utakuwa unanunua unga/mchele mboga zipo bustanini.
6. Mwili wako utakuwa unaupa mazozezi kwa kulima bustani na kuhudumia mifugo.
7. Ubongo utakuwa unachangamka kila siku kwa kubishana bei na wateja, mifugo inapopata changamoto kama maradhi, mboga zinaposhambuliwa na wadudu n.k.

Kwa wale wenye ujuzi wa ufundi hakikisha unakuwa na kijiwe cha ufundi au upo chini ya mtu mwenye kandarasi za mara kwa mara ili uwe unapiga deiwaka. Kitendo cha kuendelea kufanya kazi kinaupa mwili nguvu ya kuendelea kuishi kwa miaka mingi Kuna mzee namfahamu alikuwa fundi akastaafu 1984 akaendelea na deiwaka zake za ufundi huwezi amini amekuja kushindwa kutembea mwaka juzi tu hapa. Mafundi wenzake wote aliostaafu nao wameshatangulia mbele za haki wengine miezi michache tu baada ya kustaafu. Wengi kilichowaondoa ilikuwa ni unywaji wa pombe na kuachana na kazi ya ufundi na kuamua kukaa kula mafao na kuridhika na pesa walizokuwa wakitumiwa na watoto wao. Sasa hivi huyo mzee akitoka nje anatumia wheelchair lakini hana maradhi yoyote yanayotishia maisha yake isipokuwa tu presha ya kawaida ambayo anameza dawa kila siku na yupo poa kabisa. Na bado kumbu kumbu zake sio mbaya japo kidogo sasa hivi zinaanza kupunguwa.
Mzee kapiga 100 huyo.
 
Naamka asubuhi nakunywa maji ya vugu vugu kama glass tatu......

Napumzika kidogo alafu naenda jogging nakimbia kama km kadhaa......

Nikirudi nyumbani napiga push up kama 100......

Alafu naenda kuoga napata kifungua kinywa then...... naenda kwenye harakati...........

Jioni nikirudi napitia kijiwe cha gahawa kuchangamsha mdomo then narudi home naruka kamba kadhaa ili nitoke jasho kisha naenda kuoga alafu napumzika huku nikiangalia TV nikusubiri msosi wa usiku.........

Wanga kidogo matunda na mboga kwa wingi na mtindi kisha kulala........

😃😃😃😃😃😃😃😃😃🚚
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji598]
Tawire mkuu.
sore maji vuguvugu ni therapy au ni swaga tu?
 
Kuamka
Kunywa chai
Kwenda kununua gazeti
Kulisoma
Kula cha mchana
Kumalizia kusoma gazeti
Kula cha jioni
Kuangalia taarifa ya habari
Kulala
Hii ni ratiba ya kila siku ya baba yangu. Ni mstaafu tokea mwaka 2009. Akikosa gazeti au kitabu cha kujisomea anahisi kuumwa. Sema yeye ni muislam kwahyo hapo katikati kuna ratiba ya swala pia[emoji119]. Ana miaka 75 na afya iko njema kabisa.
 
Ndio ni ratiba ya siku nzima kutoka mawio hadi machweo. Nataka kujifunza kitu.

Pia kama mstaafu ni wewe mwenyewe sio mbaya ukashare pia.

Sharing is caring.
Kustaafu kwa TZ ni kama suspention usipokuwa makini.

Iko hivii: kitendo cha kukabidhi ofisi mstaafu hutengwa mazima na mazingira uliyoyazoea na kukulia kwa miaka nenda rudi.

Unapopata ajira ukiwa kijana mdogo, let say 20-25 na kustaafu ukiwa na 60, maana yake miaka uliyoishi kazini ni kipindi kirefu sana kuliko vipindi vingine maishani mwako ulivyoishi kabla na vilivyobaki utakavyoweza kuishi mbeleni, hivyo ofisi ni zimwi litakalobakia kichwani mwako kwa maisha yote yaliyosalia.
.
Hili badiliko la maisha kwa mstaafu lapaswa kutunishiwa misuli namna ya kulipokea ili kulikubali kwa ajili ya afya ya mwili na akili,(wengi hapa ndipo wanapofeli).

Tatizo la binadamu la kulewa sifa pamoja na adabu za bandia kwa ajili ya madaraka wanazopewa ofisini hudhania kuwa ni stahili ya maisha yao yote, na hiki ndicho kiini cha mzizi wa fitina kwa wastaafu waliowengi, kwa kuwa wanapostaafu huvikosa.

Mtu anapostaafu kwa umri mkubwa hujikuta kapoteza mambo mengi yaliyokuwa yakimpa furaha, faraja na ari katika maisha yake ya kila siku: ambapo watoto wake tayari watakuwa walishakua na kujitegemea, kwa sasa hatakuwa na mtoto nyumbani kwake.

Mke aliyemuoa akiwa msichana, sasa anaitwa ni bibi mtu ana wajukuu, hapelekeshwi ovyo na anastahili utulivu kama wa mstaafu mwenyewe.

Aliyoyazoea ya kazini, kuamka mapema, akifika kazini anaheshimiwa na kunyenyekewa, vyote hivyo 'kwaheri'.

Michongo ya ofisini na marupurupu, simu za madaraka hapigiwi na havimstahili tena.

Haya sasa yupo nyumbani kwake bila ya kazi yoyote wadhani maisha yatasonga?

Kabla ya miaka mitano ya kustaafu kwake, yampasa achague kazi mbadala utakazozifanya baada ya kustaafu na azipractise ili kuzizoea mapema.

Kama ni kilimo ama biashara ndogo ndogo azizoee kiukweli ndiyo zitakazomfanya aishi, si kwa ajili ya kipato bali ni kwa sababu ya mpangilio wa ratiba za kazi hizo kuzifanya.

Asipange mambo makubwa ya maendeleo ya kustaajabisha kichwani mwake atakayoyapata kwenye ustaafu, mawazo ya aina hii hupelekea wastaafu wengi kukwama na kutapeliwa., afanya miradi midogo midogo inayoweza kukua.

Kwa hiyo ratiba zake za kila siku zifuate mipamgilio ya miradi yake aliyojianzishia.

Kama ni duka, aamke mapema kulifungua na achelewe kulifunga, ikiwezekana duka hili liwe ni la nyumbani kwake ili kuepuka kusongamana mabarabarani kila uchao.

kama ni mifugo, aamke mapema kuihudumia, kama ni shamba ama bustani ni hivyo hivyo.

Akitoka huko kama ni shamba ama kwenye mazizi ya mifugo, apate kifungua kinywa na kupumzika.

Asipende kula sana mavyakula matamu matamu kwa ajili ya ulinzi wa afya yake, inaeleweka wazi namna umri unavyosonga ndivyo kinga za mwili zinavyopungua na magonjwa nyemelezi yasiyoambukiza yasababishwayo na lishe huweza kuibuka uzeeni.

Mambo mengine sasa ni hoby na kipaumbele cha mtu atavyopenda kuishi.

Hiyo summary nimeelezea maisha yangu ninayoishi baada ya kustaafu miaka kadhaa iliyopita.
 
Back
Top Bottom