Naweza kuorodhesha mazuri ya huyu Mama ,hasa kwa awamu yake hii ya 6!.kimtazamo wangu na uzoefu katika mambo kadhaaa,kwasababu wengi wanatajaga kasoro ngoja mimi leo nitoe maua yangu kwa mambo kadhaa si vibaya kuonesha wapi pamekwenda sambamba na heri kwa wengi.!
Lakini ukweli unabaki palepale:
kuna juhudi, kuna mabadiliko, na kuna matumaini.
Ajira: Nafasi Mpya, Watu Wanaajiriwa Kila Siku
Tunaiona Serikali ikifanya kazi kubwa kuhakikisha vijana wanapata ajira.
Fursa ziko wazi, taasisi zinatangaza nafasi, watu wanaajiriwa kila leo. Hili ni jambo ambalo kwa miaka ya nyuma lilikuwa gumu sana.
Ajira haikuwa rahisi , sasa kuna mwanga.
Wafanyakazi: Miaka 6 Bila Ongezeko ,Hatimaye Sauti Zikasikika
Wafanyakazi wengi waliteseka kwa zaidi ya
miaka sita bila ongezeko la mishahara, licha ya thamani ya pesa kupungua. Ilikuwa ngumu – hali haikuwa rafiki. Lakini sasa,
annual increment imerejeshwa.
Ni hatua ndogo, lakini ya kishujaa.Inaonesha moyo wa uongozi wa sasa wa
kuheshimu wafanyakazi na jasho lao.
Madaraja: Miaka ya Kungoja Hatimaye Imefika Mwisho
Tuliona watu
wakikomea kwenye madaraja yao kwa zaidi ya miaka sita. Hakukuwa na mwelekeo wa wazi. Sasa mambo yamebadilika ,
watu wanapandishwa madaraja kwa haki, bila kufungwa na urasimu usio na tija. Hili ni jambo la kupongezwa kwa dhati.
Mazingira ya Kazi: Nafuu Imeletwa, Heshima Imerudi
Hapo awali, mazingira ya kazi kwa baadhi ya watumishi
yalikuwa ya kudhalilisha ,hayakuwa rafiki hata kidogo. Leo hii,
hali imeanza kubadilika. Kuna utulivu, kuna heshima, na
watu wanafanya kazi kwa raha, si kwa presha. Ni mwanzo mzuri wa kutengeneza taifa lenye ari ya uzalendo.
Afya: Mapambano Kimya Kimya, Lakini Yenye Matokeo Makubwa
Katika sekta ya afya, Serikali imekabiliana na changamoto
kubwa sana: milipuko ya
Corona,
Marburg, na mengineyo. Tuliona dunia ikiyumba , lakini sisi
tulivuka salama. Hili halikufanywa kwa maneno makali ,lilifanyika kwa vitendo,
kwa vita tuliyopigana kimya kimya. Hatutakiwi kupuuzia, bali kuthamini.
Elimu: Fursa Zipo , Ukitaka Kusoma, Sasa Ni Juu Yako
Elimu leo hii
inapatikana kwa yeyote mwenye nia. Siku hizi, mtu akiamua, anaweza kusoma hadi vyuo vikuu bila vizingiti vingi. Hili ni jambo lililoanza zamani, lakini sasa limeimarika zaidi.
Mtoto akinyea kiganja,hatukikati, tunakisafisha (hasa kwa wale waliopata mimba wakiwa mashuleni). Na sasa elimu inasafishwa, inaimarishwa, na
watu wanasoma kwa bidii.
Hitimisho: Kazi Bado Ipo,Lakini Mwelekeo Ni Sahihi
Awamu ya 6
imepambana na changamoto kwa namna ya kipekee. Kuna mambo bado, lakini kwa macho ya haki,
kuna kazi imefanyika. Tuendelee kuunga mkono, kutoa ushauri wa kujenga, na kujivunia hatua zinazopigwa.
Mbele yetu kuna matumaini makubwa.
~Chavalikungu hapa!!