Nilibahatika kushiriki chaguzi zote za uraisi wa Dr Jakaya Kikwte, si muda wake kusema nilimpa kura au la huu ni wakati wa kuelezea ninavyomuona mimi raisi wetu huyu. Tukiachana na ushabiki wa kisiasa huyu mzee si mtu mbaya na si dhaifu kiasi ambacho watanzania tumekuwa tukifikiria, kiukweli Dr Jakaya ni mtu muungwana sana na ni mpole sana. Tukilinganisha awamu mbili tu ya raisi Mkapa na ya Kikwete utapata ukweli ya kuwa Mkapa alikuwa mbabe sana na hakutaka kusikia wala hakuwa na muda wa kumhurumia mtanzania. Kwa sasa watu tunamsema raisi, wanahabari wamekuwa wakiandika kwa uhuru kiasi si kama awamu iliyopita. Kuhusu hii sintofahamu inayolikumba taifa letu, nahisi raisi wetu anadanganywa, anapewa taarifa zisizosahihi! Ninakuewaa na mashaka kwa ninavyomjua huu mzee, hali inayolikumba taifa letu, watu wanaanza kutoa maneno yanayoweza kuleta hatari zaidi ya kumaliza tatizo tena bungeni! Taarifa ya serkali iliyosomwa na Mh Lukuvi inatia shaka kama ni ya serikali au ni ya Lukuvi mwenyewe! Mh huyu alisema askari walikuwa wamkamate mtu aliyerusha bomu lakini walizuiwa na wananchi kwa kupigwa mawe hivyo wakashindwa kufanya kazi yao wakaanza kujihami! Kwa akili hta ya mtoto wa darasa la kwanza, hivi inaingia akilini mtu kaptwa na janga uende kumsaidia aanze tena kukushambulia!? Kweli jamani, ndugu yangu Kikwete kweli? Hizi taarifa umezipokea au hata hujaambiwa? Binafsi naomba kupingana kabisa na mh Lukuvi, bado naamini Dr. Kikwete sasa ni wakati ambao uliwaahidi watanzania kuwa utwashangaza kwa kukumbukwa kwa mazuri, upole wako unatumiwa vibaya na wasaidizi wako. Nakataa kabisa kuwa wewe si dhaifu,bado naamini kuwa unaweza kufanya maamuzi ya kukumbukwa ukitumia akili yako na kuachana na ushauri unaokupoteza! Nilimsikiliza kijana wako Nape pia, hapa napo nilipatwa na simanzi, hivi Nape anamaanisha wakatoliki pia walijirushia bomu pale kanisani? Hivi kuna ulazima gani wa kuweka propaganda sehemu ambayo hahihitaji propaganda!? Ifikie wakati raisi wetu awakatae hadharani hawa aliodhani wangemsaidia lakini wamegeuka kumsaliti. Watnzania hatutaki propagnada, tunahitaji maendeleo. Siasa ziishie majukwaani lakini ofisini iwe utendaji. Nashauri mheshimiwa Kikwete bado uko na nafasi ya kuonyesha watanzania kuwa walikuamini na unauwezo wa kuwahakikishia usalama kwa kukataa maneno ya kupikwa, twende kwenya ukweli. Watu wa Arusha waliokuwa kwenye mkutano wanaujua ukweli wa kilichotokea, Lukuvi katoa tamko kwa haraka sana sidhani kama kafanya upembuzi yakinifu wa hayo maneno yake. Naamini kama hatutaweka mambo ya kisiasa, sintofahamu hii itapata jibu kwa vile Mungu wetu hataacha wenye haki wahangaike.