Nionavyo mimi kwa francis cheka na soka la bongo.

Nionavyo mimi kwa francis cheka na soka la bongo.

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
NIONAVYO MIMI KWA FRANCIS CHEKA NA SOKA LA BONGO.

Bondia wetu CHEKA hivi karibuni alitangaza nia yake ya kujiendeleza kielimu.Ataanza na pre-form na baadae mpaka chuo kikuu,binafsi namtakia kila la kheri.

Anachofanya CHEKA ndicho tunachoshindwa kwenye soka,hatuna CREDITS na hatutaki ku-resit wala kurudia darasa kabisa.kuna uwezekano CHEKA akafika form four kabla ya sisi kucheza AFCON!

Ni rahisi kwa Francis Cheka kwenda chuo kikuu kuliko TAIFA STARS kucheza kombe la Dunia,Ni rahisi kwa Francis Cheka kupata PHD kuliko STARS kutwaa kombe la AFCON,Ni rahisi kwa CHEKA kuwa professor kuliko STARS kutwaa kombe la Dunia!!

Binadamu anahitaji zaidi akili,Pesa na Elimu ni ziada tu.

I'm sorry
 
uamuz mzuri maana mastaa wengi wakishapata pesa wanajua kutanua na mademu kwa wingi!!
 
Back
Top Bottom