Nakapanya
JF-Expert Member
- May 22, 2012
- 2,096
- 709
Ule uchaguzi uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na wansoka wa Tanzania,uchaguzi uliojaa vibweka,vituko,fitina,majungu,ubabaishaji hatimaye umekamilika na viongozi wapya watakaoongoza jahazi hili la soka la Tanzania kwa miaka minne ijayo wamepatikana.
Niwapongeze viongozi wote waliochaguliwa kuanznia Raisi na wawakilishi wote,jukumu mlilokabidhiwa ni kubwa sana na linahitaji moyo wa dhati kulikamilisha kwa mafanikio.
Ukiniuliza juu ya nini nategemea kutoka kwa hawa viongozi wapya wa TFF; nitakwambia sitarajii chochote kipya katika uendeshaji wa soka wala sitarajii maendeleo yoyote katika soka letu.Nasema hivyo kwasababu sioni kiongozi yeyote aliyechaguliwa ambaye ana nia ya dhati ya kuliendeleza soka la bongo (hapa sio hawa waliochaguliwa tu,hata wale walioshindwa pia),wengi wao wanaenda pale kwa maslahi yao binafsi na si kwa manufaa ya mpira wa Tanzania.
Wagombea walitoa ahdi nyingi sana ambazo kimsingi kama zingekuwa zinatekelezeka kwa aaina ya viongozi ambao tunao basi soka la bongo lingekuwa mbali maana waliyoyaahidi si mageni yalishaahidiwa na viongozi waliopita lakin mpaka wanaondoka madarakani hamna kitu zaidi ya kupiga hela za makusanyo ya mechi za simba na Yanga.
Inanikumbusha kiongozi mmoja wa klabu moja hapa bongo,wakati wa uchaguzi aliahidi kuwajengea uwanja timu yake lakini miaka kadhaa alipokuja kuulizwa juu ya ahadi yake akaruka kimanga na kudai hawez kujenga uwanja ndani ya miaka michache,ukiangalia mfano huo ndio nanavoona pia kwa hawa viomgozi wapya wa TFF waliochaguliwa.
Mwisho niseme watanzania hususani wapenda soka wana imani kubwa na nyinyi hivyo ni jukumu lenu kwafurahisha Watanzania au kuwaangusha.
Cc: Jamal Malinzi