Natangulia kuwapa pole watakokuja kulalamika kwamba kumbe bora Tenga kuliko Malinzi. Ni hatari, kama sio ujuha, kujipa matumaini kwa uongozi usio na track record kama huu wa Malinzi. Sijui nilaumu katiba ya TFF au wadau wenyewe, lakini nchi kama hii ambayo kila Uchaguzi Mkuu tunakuwa na wagombea si chini ya sita wa urais wa nchi, kuwa na wagombea wawili tu wa urais wa TFF ni ajabu kama sio uchuro. Kadri wagombea wenye sifa wanavyokuwa wengi ndivyo uwezekano wa mmoja aliye bora unavyoongezeka, ingawa bado ni 'trial and error'. Lakini huu wa wagombea wawili ni 'error and trial'.