Nionavyo kuhusu babu wa loliondo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nionavyo kuhusu babu wa loliondo

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by GIRAY, Mar 22, 2011.

 1. G

  GIRAY Member

  #1
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza nawasalimuni. naomba nisionekane nimepitwa na wakati kwa kuchangia mada kumhusu huyu mzee. ila kutokana na maoni mengi ya watu nalazimuka kutoa maoni yangu. Wengi, hasa watu wanaodhani wanayajua maandiko ya biblia wamemshambulia sana babu. Hoja kuu ni kwamba
  moja kwanini atoze fedha, pili kwanini atumie mitishamba, tatu kwanini wengine wafe kabla ya kupata dawa, nne kwanini hahubiri na kuwaelekeza watu kwa mungu.
  dhana yote hii kwangu si ya msingi sana kwa sababu zifuatazo.

  Mimi hua naamini Mungu anahusika na uponyaji kwa mtu hata kana amekwenda kutibiwa Hospitali. na huko huwa watu hawahubiriwi wala kuombewa bali hupewa tu dawa na kisha Mungu akaendeklea kuahudumia. Hatahuko watu wengine huwa wanakufa pamoja na kupata dawa. Babu anaweza kua mmoja wa watu ambao mungu amewainua kuto huduma kama ya Hospitali na ndo maana haombei watu.

  Wengi wanaompinga walitaka kama kweli Mungu amemtuma kuponya basi angefanya kama kina fulani na fulani, lakini Mungu si mdogo hivyo.

  suala la kutoza fedha si tatizo kwani kama kaambiwa na aliyempa dawa afanye hivyo, basi Mungu anakazi na hizo fedha wanazochangia watu, hilo haliwezi kuwa kigezo cha kuona kama hakutumwa na Mungu.

  Wengine hutoa hoja kua kwanini hata wazinzi na wenye dhambi wanapewa dawa. Huu ni ujenga zaidi, kwani hao hao wanaosema hivyo mara nyingi utawakuta wakiombea wagonjwa, wasafiri,viongozi nk bila kujali kama wameokoka au la! na baada ya maombi huamini kabisa kua Mungu amesikia maombi yao. kwanini babu akifanya hivyo kutoa huduma kwa wote iwe tatizo?
  suala la kutumia miti nia sawa tu na wataalamu wanaotibu hospitali wanavyo tumia mimea kutengeneza dawa mbona hatuhoji, au kwa vile huyu mtanzania
   
Loading...