Ninyi viongozi wa umma mnaochapa watu viboko mnawachapa kwa mamlaka gani?

baada ya kuua akapakia maiti kwenye gari na kwenda mwenyewe kituo cha polisi! R.I.P Mwavindi! Viongozi wanatuona Watz mazuzu......
 
baada ya kuua akapakia maiti kwenye gari na kwenda mwenyewe kituo cha polisi! R.I.P Mwavindi! Viongozi wanatuona Watz mazuzu......
Tena alipakia "mzoga" wa RC huyo kwenye gari ya serikali na kuiendesha mwenyewe hadi kituo cha polisi. Hiyo gari ndiyo hiyo hiyo iliyokuwa imetumiwa na RC huyo kwenda shambani na nyumbani kwa Mwamwindi na kumdhalilisha mbele ya familia yake. Kufika polisi akawaambia "nimewaletea huo mzoga wenu".
 
Na wanaochapwa nao ni umbwa kama umbwa zingine! Unaruhusuje ujinga kama huo?
 
Utawala wa mkono wa chuma ndiyo ulivyo, uongozi wa wananchi haufanyi hivyo kwani uko pamoja nao.
 
Wapo wengi sana,hawakosekani.
Kuna mmiliki wa kiwanda barabara ya Pugu aliwatandika viboko wafanakazi wake na haikushangaza baadhi ya wafanyakazi walishangilia! Unategemeaje waandamane kudai haki zao!
 
Nimekaa sit ya mbele ili nimuone mmiliki wa kile kitega uchumi anachapwa mijeredi, sijaona: hii ni adhabu ya bidagaa
 
Tuseme ukweli ndugu yangu,hivi kupigwa viboko kumi hadharani na kuingizwa mahabusu ukaozee huko miezi mitano hadi sita huku DPP na hakimu wakikupiga danadana (DPP-Nategemea kubadilisha mashtaka,Hakimu-Leo hayupo anaudhuru) ni kipi bora?
Kuna watu wangeweza kumnasa makofi huyo waziri lakini busara inatawala wanaona ngoja waumie kidogo kwa muda mfupi kuliko ukaozeee rumande
 
Serikali Ninayoiongoza Mimi Halitakuwa Na Michakato, Hata Kama Ni Samaki Unachakata Itaozea Mkononi
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
Hiyo sio busara,kumnyamazia mtu anayekuonea na kushindwa kumchukulia hatua kunatokana na uwoga na unyonge tu si busara
Unajua neno "hali halisi?"
Kwenye kipindi cha kampeni nilikutana na kijana mmoja alipita bila kupigwa kwenye udiwani kupitia CCM.Nilimuuliza "unajisikiaje kupita bila kupingwa wakati wagombea wenzio wameenguliwa kwa mambo madogo madogo,huoni kama kuna watu wamenyimwa haki"?".Majbu ya kijana yule (Mhitimu wa UDSM) yalinistua lakini yamekuwa yakinijia mara kwa mara na yamenifumbua macho.Alisema "Mzee ukiwa unaitafuta haki utakongoloka mpaka unaingia kaburini,hakuna haki katika siasa".
HITIMISHO-Hivi kweli unaweza ukajibishana na askari ambaye kwa kumuangalia usoni tu anaweza kuachia risasi?
 
Ungekuwa wewe uulizwe kuchapwa viboko na kwenda jela unachagua nini? Ungesemaje,huoni kwamba kuchapwa viboko wamesaidiwa? Kwanini ukaanze kusumbua polisi na mahakama wakati unaweza ukawapa adhabu hapo hapo.
 
Halafu jiulize kwanini kipindi hiki cha jiwe ndio sana? Kuficha maana yake watu wasijue na kama hawajui maana yake hawezi toa msaada wowote ule,

Nazani wanaogopa wananchi wakitoa msaada wa maombi utaharibu mipango yao, Nazani mnakumbuka yale maombi ya Lisu, maana ndio yaliyomponya, sasa hawataki kurudia kosa, ndio maana mambo yanaenda kimya kimya, nyie mnapewa taarifa ya kifo tu.
 
Tunazo mahakama za gachacha, wanao fanya uharifu kama ulio usemana mwingine mwingi unao fanya na polisi, jet nk, wanajua kuwa wanavunja sheria, lakini wanajua mahakamani hawatafikishwa, na wakifikishwa hawatafanywa lolote.
 
Mimi siku aje Boss wangu anichape viboko! Sitakubali zitapigwa mpaka tugawane nyumba za Serikali kama sio mimi basi yeye ataenda Polisi kuchukua PF3 akatibiwe Hospital na mwingine atalala mahabusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…