Ninunue kiwanja au nianzishe biashara kwanza

Nyamwage

JF-Expert Member
Oct 16, 2020
634
1,535
Nina kiasi cha pesa na nimekua njia panda nini nifanye cha kwanza ninunue kiwanja au nifanye biashara nikipata faida ndio nianze mipango ya kununua kiwanja maana kibaruani nimeachishwa.
 
Unategemeana na mazingira yako, kama unataarifa za kutosha na umejiridhisha kwa asilimia kubwa kuwa biashara itazalisha basi ni vizuri kufanya biashara, vinginevyo ni heri ukachukua eneolako atleast litakua linakupa hisia zamafanikio.
 
Nunua kiwanja afu kiache...tafuta zingine ndo uanze biashara mdogomdogo hapo hata kujenga ukitaka ni easy.
 
MAELEZO ULIYO TOA HAYATOSHI KUSAIDIWA... LAKINI ogopa zero return investment hebu fikiria una 10M tu halafu pesa yote umenunua kiwanja... na umesema kibarua kimeota nyasi... HICHO KIWANJA KITAKUSAIDIAJE.
 
Tafuta Asset kwanza kabla ya kuwa na Liabilities. Anzisha walau Biashara mbili ndogo zitakazokuingizia kipato chochote cha kila siku kisha simamia vizuri, mengine yatafuata.
 
MAELEZO ULIYO TOA HAYATOSHI KUSAIDIWA... LAKINI ogopa zero return investment hebu fikiria una 10M tu halafu pesa yote umenunua kiwanja... na umesema kibarua kimeota nyasi... HICHO KIWANJA KITAKUSAIDIAJE.
eti 10M
 
Nina kiasi cha pesa na nimekua njia panda nini nifanye cha kwanza ninunue kiwanja au nifanye biashara nikipata faida ndio nianze mipango ya kununua kiwanja maana kibaruani nimeachishwa.
Kama umesimamishwa kazi basi wewe uko katika vulnerable group.Uamuzi wowote unaofanya sasa hivi unaweza kuwa na negative consequences.Ila jiulize changamoto yako kubwa kwa sasa nini?Then jiulize fursa kubwa uliyo nayo ni ipi.Namna hii utaweza kuamua iwapo sasa ni wakati sa hihi wa kufanya uamuzi wowote.

Kila la heri
 
Sikujui Hunijui...Nunua kiwanja kijana mengine yatakuja. Hata hasira za mafanikio zitakujia ili
Ujenge....

Bakiza kiasi nunua bodaboda endesha mwenyewe...Hutojuta
Na kama upo level flani ya maisha nunua town ace pick up / kirikuu / guta pikipiki ingia kijiweni endesha mwenyewe...inshort fanya logistics biz ila kwa kigezo cha kuendesha mwenyewe sio umpe mtu akuletee hela.

Nimekuchukulia kwa kawaida sanaa na kukushauri very widely cz sikujui vizuri au sijui utaftaji wako upo level gani. Otherwise fanya nachokuambia.
 
Anza na biashara lakini biashara inahitaji plan nzuri....

Kama unanunua kiwanja hakikisha ni sehemu ambayo mtu anauzia shida na kimekaa sehemu ambayo ukikinunua miaka kadhaa thamani yake itakuwa kubwa sana

Usigeenda kuzika hela sehemu porini halfu uka mjini kutafuta hela.

Kuna dogo alinifuata amepiga deal ya 1.3M anataka aanze kujenga kijijini kwako taratibu taratibu huku anaendelea na kazi.Nikamuuliza hiyo nyumba ikikamilika utaenda kukaa, akasema kazi ikiisha nitarud home.Nikamuuliza M1.3 nyumba itafika wapi? Akasema kwenye renta maana ni vyumba vitatu tofauli za kuchoma(tshs.100).

Nikamwambia acha uoga kabla ujawa na kazi hii ulikuwa boda boda,nunua pikipiki used mpe mtu akupe pesa hlf kila mwezi ongezea mshahara,Jenga huku pesa inaingia.Nahisi dogo alikuwa na zile akili za kijijini Mtu nyumba basi akajenga ikafika juu ya dirisha, Hela ikakata.Miezi miwili mbele bahati mbaya akafukuzwa kazi hata budget ya miezi 2 mbele na mkewe hana, kanifuata kuniomba ushauri.Mi ni kamwambia si urudi kwenye boda boda pikipiki si unayo kumbe hela alienda kujengea.Hii ni tofauti ya kuzika hela na kutumia pesa kutengeneza pesa

Sasa huyo alikuwa 26 yrs sijui wewe una umri gani ila plan za kuingiza hela ni muhimu sana kuliko kuzika hela wkt huna sehemu za kuingiza pesa za uhakika
 
Back
Top Bottom