Ninunue gari la aina gani kwa bajeti ya 6M

Danny Massawe

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2012
Posts
1,299
Reaction score
765
N dugu wana JF, nawasalimu nyote. Nipo kny hili jamvi kwa muda na nimejifunza mengi, leo kwa mara ya kwanza nimepata ziada ya kipato na nina Tsh.Milioni 6 na ningependa kuifanyia hii pesa kitu cha kukumbuka baadae nikije nikaitumia hovyo, nimeamia makazi mapya hivi karibuni na kunaumbali kidogo na kazini/mjini hivyo mimi na familia huwa tunapata tatu ya kupanda bodaboda, hivyo nimeamua kupeleka hii pesa kwenye kununua usafiri. Nawaomba ushauri ndugu zangu ninunue gari ya aina gani ambayo itanifaa ??
NB:
1.Nina familia ya watu watano
2.Kila siku natembea zaidi ya km 30
3.Barabara ninapoishi ina ni mbaya iko rafu lakini haina mashimo makubwa
4.Bajeti ni million 6
5.Wakati wa sikukuu huwa natoka Mtwara mpaka nyumbani kwa wazazi Arusha.
6.Ningependa gari inayotumia mafuta vizuri na linalodumu
7.Ninaishi Mtwara mjini
Naombeni ndugu zangu mnipe ushauri ambao utakuwa na manufaa kwangu. Ninunue gari gani na h ii million 6?
ASANTE
 
mkuu ongeza kidogo uagize toyota carina TI itakufaa sana kulingana na maelezo yako hayo..
 
asante kwa ushauri, kuagiza carina ti mpaka bongo inafika milioni ngapi??
 
Mkuu ongeza kidogo nikupe Toyota Ipsum new model,inabeba watu 8 pasipokubanana n'a dereva!!
 
Carina ti ni 7.5 lakini kwa route yako sidhani kama itamudu.
nishauri kaka ninunue gari ya aina gani ??maana route ya mtwara-arusha ni ndefu sana na ile ni gari ndogo hata kwa usalama haipendezi
 
Mkuu ongeza kidogo nikupe Toyota Ipsum new model,inabeba watu 8 pasipokubanana n'a dereva!!
mkuu asante kwa ushauri na pendekezo..ila nauliza ipsium inaweza route ndefu na kuvumilia rough road?? ila nitaendelea kutafiti.
 
Haya nipe 7.2m kwa hii Daihatsu Terrios Kid

Watu 5, immaculate condition
Engine ndogo cc 650 lakini very powerful coz ni turbo charged
 
Nunua gari itakayokuingizia na kipato pia kama hutojali!!! Chukua suzuki carry!!!!
 
mkuu asante kwa ushauri na pendekezo..ila nauliza ipsium inaweza route ndefu na kuvumilia rough road?? ila nitaendelea kutafiti.

Mkuu Ipsum new model ni bonge la gari,ina 4wheel so rough road sio tatizo kabisaa!!!!
 
Ongeza hela ununue RAV4 old model itakufaa sana.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
nashukuru kwa ushauri wenu wenye thamani, nimependa zaidi walionishauri escudo v6 na rav 4 old model...ila kwa bajet ya 6m nitapata aina hi ya magari? au nivute subira mpaka ifike milion ngapi?
 
Kwa RAV4 old tafuta 14 unapata nzuri kabisa ambayo utaanza kuitumia wewe kwa hapa bongo na usajili kwa jina lako.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
N dugu wana JF, nawasalimu nyote. Nipo kny hili jamvi kwa muda na nimejifunza mengi, leo kwa mara ya kwanza nimepata ziada ya kipato na nina Tsh.Milioni 6 na ningependa kuifanyia hii pesa kitu cha kukumbuka baadae nikije nikaitumia hovyo, nimeamia makazi mapya hivi karibuni na kunaumbali kidogo na kazini/mjini hivyo mimi na familia huwa tunapata tatu ya kupanda bodaboda, hivyo nimeamua kupeleka hii pesa kwenye kununua usafiri. Nawaomba ushauri ndugu zangu ninunue gari ya aina gani ambayo itanifaa ??
NB:
1.Nina familia ya watu watano
2.Kila siku natembea zaidi ya km 30
3.Barabara ninapoishi ina ni mbaya iko rafu lakini haina mashimo makubwa
4.Bajeti ni million 6
5.Wakati wa sikukuu huwa natoka Mtwara mpaka nyumbani kwa wazazi Arusha.
6.Ningependa gari inayotumia mafuta vizuri na linalodumu
7.Ninaishi Mtwara mjini
Naombeni ndugu zangu mnipe ushauri ambao utakuwa na manufaa kwangu. Ninunue gari gani na h ii million 6?
ASANTE

Tafuta Passo ya 2004-2005 bei 6.5M kuingiza hapa bongo barabarani
 
Mkuu hiyo Ipsum bei gan? Na je imetumika bongo kwa mda gani?

Mkuu bei ni 10 mln though negotiable kidogo,imetumika bongo mwaka mmoja n'a miezi miwili,ni pm namba yako kwa info zaidi!
 
nashukuru kwa ushauri wenu wenye thamani, nimependa zaidi walionishauri escudo v6 na rav 4 old model...ila kwa bajet ya 6m nitapata aina hi ya magari? Au nivute subira mpaka ifike milion ngapi?

mkuu,ongeza mia tano hapo kwenye bajeti yako nikupe rav 4 old model ipo katika hali nzuri kabisa,kama uko poa nitafute pm.
 
asante mkuu nitajitahidi kutafuta iyo 500k, ila ningepena kujua iyo rav 4 ni ya mwaka gani, rangi, imelipiwa na ina matatizo gani makubwa yakurekebisha na ila kusahau picha ingesaidia sana
 
Back
Top Bottom