BANGO JEUPE
JF-Expert Member
- Nov 21, 2015
- 3,079
- 2,152
Tumelelewa katika mazingira tofauti. Tunalea na wengine tuna mpango wa kulea ila wengi tunalea watoto wetu bila mfumo mzuri utakaowaongoza katika maisha yao.
Malezi uliyopitia yameathiri vipi mahusiano yako kijamii na maisha kiujumla?
- Mzazi, kama lugha unayoitumia kwa mwanao ni matusi ujue unacho cha kumfunza.
- Tabia za kike na kiume ni zipi na humuoneshi mipaka. Jua unacho cha kumfunza.
- Humsikilizi na kuheshimu mawazo yake. Jua unacho cha kumfunza.
- Uko bize na hujali kitu katika malezi yake. Jua umekosa cha kumfunza ila yuko anayemfunza.
Malezi uliyopitia yameathiri vipi mahusiano yako kijamii na maisha kiujumla?