Nini umuhimu wa RECOVERY disk?

Void ab initio

JF-Expert Member
Mar 1, 2015
5,720
5,659
Nimenunua Laptop HP mpya inapartition yenye Recovery, na inanitaka niihamiashie kwenye external disk.
Je, nini kazi au umuhimu wa Recovery disk?
 
Recovery disk inafanya kazi ya ku-restore state ya kompyuta yako kama ulivyoikuta mwanzo hasa pale yatakapotokea matatizo kwa mfano, bahati mbaya hard disk imecheza, na kompyuta inawaka lakini haileti screen ya windows (inakua tu black). Mfano mwingine ni pale unapopata virus au pale windows yenyewe tu ikashindwa kuwaka.

Sasa, kwa kua ndio unaanza kutumia hiyo kompyuta, recovery ya muda huu ulivyoikuta haina maana sana manake hataitaweza kurudisha state ya kompyuta yako kama vile ulivyoitumia, isipokua kama vile ulivyoinunua Siku ya kwanza. So unaweza kui-delete lakini, nakushauri baada ya Kuweka softwares na vitu vyote vya msingi, tengeneza recovery nyingine ili incase Siku kompyuta imezingua, una back up ambayo itarudisha sio tu windows, ila mpaka files Na software ambazo uliziweka wewe baada ya manunuzi ya kompyuta.

Siku kompyuta ikisumbua na kushindwa kuwaka itakupa option mbili, 1. To restore, kwa kutumia recovery disk
Au 2. Ku-format hard disk
 
Back
Top Bottom