Nini ukweli kuhusu mishahara hewa?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,634
7,015
Hadi sasa sijaona afisa utumishi,mhasibu wa serikali za mitaa wala wa hazina wakiwajibishwa kwa wizi wa mishahara hewa kama tunavyosikia kila kukicha. Je ni kweli kabisa kuna watu walilipwa mishahara huku wakiwa si watumishi halali?Au ni aina mpya ya siasa?Maana nilisikia kuna mtu alikuwa anaiba mil 7 kila dk tangu 2012,ukipiga hesabu jibu la hela aliyoiba hata calculator inagoma kutoa jibu? Hiyo nikajua nisiasa tu! Je hii nayo ni siasa?
 
Mishahara hewa??? Kijana nimekuelewa.. Hao maafisa rasilimali watu/utumishi cjaoja hata mmoja ambae amewajibishwa.. Kwan katka uajiri mkurugenz wa jiji/mji/halmashaur hausiki?? Hii michezo ya siasa za viini macho na kutaka sifa zinatumaliza tanzania
 
Hata mimi nashangaa hasa kuhusu hilo la mtu kuvuna 7m kila baada ya dakika moja kwa miaka yote hiyo. Is it turuuu?
 
Inashangaza sana kuona wanaoajibishwa sio wale waliosababisha kuwepo kwa watumishi hewa, wao wanaendelea na vyeo vyao kama kawaida. Ushauri wangu kwa mh rais dkt JPM aanze na hawa asipoteze nguvu nyingi kutafuta watumishi hewa wakati maafisa utumishi, maafisa raslimali watu, wakuu wa idara nk hayo ndiyo majipu hatari kwa ustawi wa taifa letu la Tz.
 
14,716,800,000,000tsh kama unatumia calculator UCHWARA namba hazisomi..
Trilion 14,bilion 716, na milion 800
N:B majina ya hela yananipiga chenga
Samahani.
Swali la nyongeza.
Huyu jamaa kaweka wapi haya maburungutu yote
 
Samahani.
Swali la nyongeza.
Huyu jamaa kaweka wapi haya maburungutu yote
Aisee hapo ndo nnapopata wasi wasi na mifumo ya nchi yetu.. Hii nchi viini macho vingi sana... Watu wamepiga pesa ,kila mtu kashachukua chake...
 
Kama mtu mmoja s aweza kuiba nusu ya budget ya serikali hii si hatari kubwa sana?!
 
Ni mishahara hewa au kazi hewa.kama mishahara imelipwa nadhani sio hewa.Bali kilicho hewa ni kazi.
 
Kama ndo siasa ss walimu ndo wahanga wakuu. Maana mishahara haitoshi, vyeo havipandi, nyongeza imeondolewa. Tunachofaidika nacho ni idadi ya wanafunzi imeongezeka saaaana na sasa baadhi ya shule kuna shift, kwa hilo serikali tunaisifu kwani inatuwajibisha sawa sawa! Tunaisifu, kwani kinyume chake hata haka kadogo tutanyang'anywa!
 
Hadi sasa sijaona afisa utumishi,mhasibu wa serikali za mitaa wala wa hazina wakiwajibishwa kwa wizi wa mishahara hewa kama tunavyosikia kila kukicha. Je ni kweli kabisa kuna watu walilipwa mishahara huku wakiwa si watumishi halali?Au ni aina mpya ya siasa?Maana nilisikia kuna mtu alikuwa anaiba mil 7 kila dk tangu 2012,ukipiga hesabu jibu la hela aliyoiba hata calculator inagoma kutoa jibu? Hiyo nikajua nisiasa tu! Je hii nayo ni siasa?
Mkuu kinachofanyika sasa ni siasa za kutafuta kiki kama vijana wa sasa wanavyosema, mishahara ya watumishi wanaoitwa hewa tayari ilikuwa inarudishwa hazina(Wizara ya fedha) na halmashauri husika.Tayari uhakiki ulishafanywa zamani kama sikosei mwaka 2010 na miaka mengineyo na majina kuwepo utumishi.Kawaida kama mtumishi hayupo kituoni mishahara hurudi hazina. Ndio maana hakuna mtu au mkuu wa idara aliyekamatwa au kuhojiwa.
 
Back
Top Bottom