IshaLubuva
JF-Expert Member
- Dec 4, 2008
- 250
- 11
Wana JF nimekuwa nikipata ukakasi kuhusu matumizi ya maneno Jeneza na Sanduku la Maiti/Marehemu. Mara nyingi watu wamekuwa wakiyatumia maneno haya mawili kana kwamba yaanamaanisha kitu kimoja. Lakini mimi binafsi naamini kuwa yanamaanisha vitu wiwili tofauti:
Jeneza ni nyenzo ya kubebea mwili wa marehemu kutoka nyumbani/hospitali kwenda kwenye kaburi (kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine). Kwa kiingereza linaitwa Bier.
Sanduku la maiti ni boksi lililotengenezwa kwa ajili ya kumhifadhi marehemu ikiwa ni pamoja na kumsafirishia kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kwa kiingereza linaitwa coffin.
Tofauti kubwa kati ya Jeneza na Sanduku la Maiti ni kwamba Jeneza huwa halizikwi pamoja na marehemu wakati sanduku la maiti huzikwa pamoja na marehemu.
Waswahili karibuni kwa mjadala