Nini Tofauti ya hizi? Website and Blog | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini Tofauti ya hizi? Website and Blog

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Shinto, May 18, 2012.

 1. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Kama mmeshawahi ku-discuss hapa, naomba link!.
  Natatizwa sana na hivi vitu, website ya kawaida, web portal na blog.
  Nini tofauti yake, in terms of contents, functions and technologies used to make them.

  Shukran
   
 2. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,746
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  yani tofauti kubwa kati ya website na blog naeza kusema ni kua website ni formal na blog ni informal.

  Hizi ni tofauti chache nyengine za blog na website

  -Blog inakua updated mara kwa mara wakati website inakua updated mara chache

  -hizi blog zinakua informal zipo zipo tu na zinafanana nyingi lakini website zinakua formal tena zipo proffesional zimekua designed kwa hali ya juu

  -katika blog kuna interactive yani mtu anapost watu wanacoment na yeye anawajibu lakini katika website hamna hivi ni only communication yani mtu anaandika na we unasoma basi

  -kitu chengine website ni transactional yani unafanya manunuzi unaeka kadi ya benk wanakata hela unapata bidhaa ila blog hamna

  Mwisho naeza kusema kila mtu anaweza kuwa na blog na kila shirika na biashara inatakiwa iwe na website.

  Kuhusu portal ni aina ya site ambayo inakusanya vitu vingiiiiiiii katika sehemu moja inakua kama search engine sema inakua na vitu vingi zaidi. na sio lazima hivo vitu viwe vyao.

  Mfano wa portal ni igoogle (sio google), au yahoo.com ukiingia utaona wana games, habari, email service na madude kibao
   
 3. Achahasira

  Achahasira JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu umenena vizuri kabisa
   
 4. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu heshima mbele,
  Ahsante kwa majibu haya.
  Je waweza kwenda mbele zaidi, kama kunatofauti katika tools na scripting languages wakati wa ku-develop hizi?
   
 5. N

  Namtih58 JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 236
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwanza inaonekana unachanganya kidogo, portal na blog zote ni websites. Tofauti yazo ni matumizi.

  Blog huwa, mara nyingi ni mtu binafsi, amabpo anaweka mawazo yake binafsi, inawezekana pia watu kadha wakashirikiana, lakini inakuwa ni mawazo yao binafsi, blog nyingi huwapa wasomaji uwezo wa ku-comment, wakaandika walicho fikiria kuhusi alicho andika mwenye blog.
  Kukija kw atechnologies za kutengeneza blog, hapo sijaelewa hasa unachokitaka, programing language yoyote ambayo inaweza kutengeneza website una uwezo wa kutengeneza blog (javascript, php, c#, Ruby, python e.t.c.).

  Watu wengi hutumia "frameworks" ambazo ni websites ambazo tayari zimesha tengenezwa, kilichobaki ni kwa anaye tumia kuiboresha anavotaka yeye. Kwa mfano Wordpress [nadhani ndiyo inatumika zaidi ya zote] , Habari, FlatPress, MovableType, Drupal [CMS], jumla [CMS], DotNetNuke [CMS]. Kwa kifupi CMS (content management systems) zina uwezo zaidi ya blogs.

  Portal, kawaida ni aina ya website amabayo inakusanya mambo kutoka sehemu tofauti na kuzileta pamoja. Mara nyingi zinatumika kwenye serikali. Utapata kuna website moja ambayo mtu anaweza kuenda website(portal) moja, akapata mambo yote kuhusu mikono tofauti ya serikali mfano usa.gov. Portal zisizo za serikali ni kama AOL.

  Teknolojia itakuwa zile zile, pengine kwa portal inabidi uzi chague kwa makini zaidi, kwa kuwa inkuwa ni kubwa kuliko blog, na kazi portal inafanya ni nzito kuliko blog.
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu hata hapa na mimi umenielimisha nlikua sijui vyote hivyo
   
 7. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,746
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  Nafkir namtih kalijibu swali lako. Right?
   
 8. Ziroseventytwo

  Ziroseventytwo JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 3,515
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  ...good explanation! Satute.
   
 9. nurbert

  nurbert JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 1,925
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  xo guy kwa maelezo yenu! JAMIIFORUMS ni portal au web, na FACEBOOK je?
   
 10. N

  Namtih58 JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 236
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  JF ni website ya aina ya forum. FB ni website ya aina ya social networking.
  Elewa kuwa zote ni websites za aina fulani fulani tuu mkuu.
   
 11. w

  wade kibadu Senior Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thank na wengine tumepata elimu hiyo very beatiful muuliza swali na mlio toa majibu.
   
 12. N

  Namtih58 JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 236
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Just realised the above line kinda implies Wordpress , Habari, FlatPress and MovableType are not CMS's. Zote ni CMS ukizingatia kuwa zote zina manage content, nilichotaka kusema ni kuwa, hizi zinajihusisha na content za blog, wakati kina Jumla, Drupal na DNN, ni more generic, zinaweza kutumika kumanage more diverse content.
   
 13. nurbert

  nurbert JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 1,925
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  owkay kaka. Af tofaut ya wapsite na website. Ki It zaid?
   
 14. badshah

  badshah Member

  #14
  Dec 26, 2013
  Joined: Mar 16, 2013
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwa kifupi ni kwamba blog ni aina ya website ambayo inajulikana kama Web Log na kuchukuliwa herufi ya mwisho ya Web ambayo ni "b" na kuunganishwa na neno zima la mwisho ambalo ni Log na kuwa Blog. Unaweza kuwa umeshawahi kusikia kuhusu Static and Dynamic websites. Blog inaweza kuwa ndani ya website au inaweza pia kujitegemea yenyewe kama yenyewe.
  Ikiwa una website basi unaweza ndani yake ukaongeza blog. Na blog haiwezi kabisa kuwa website. Kutokana na Wikipedia, Blog ni sehemu ya website ambayo ina taarifa zenye kuongezwa na kubadilishwa kila siku huku kukiwa na nafasi ya watembeleaji kuweka maoni yao juu ya mada unazoandika humo.
  Blog huwa mara nyingi zina taarifa nyingi mbalimbali na huwa mpya (up to date) kila siku kwani mwenye blog anakuwa akiongeza taarifa kila siku au kwa muda maalum. Na lugha inayotumika sanasana inakuwa ni rahisi na yenye kueleweka na pia taarifa zake ni rahisi kuzitafuta kwani huonekana katika Blog Achieve.
  Katika Blog kuna kitu kinaitwa vipachiko (Posts). Kila post ina page yake inayojitegemea Lakini page kuu (main/ home page) ya blog inakuwa ina muhtasari wa mada za karibuni za Blog hiyo na kila mwisho wa mukhtasari utaona neno Read More ambapo ukibofya hapo ndiyo inakupeleka katika ukurasa maalum wa mada hiyo peke yake.
  Kitu kingine ni kwamba, katika blog huhitaji kutengeneza ukurasa kwaajili ya mada unayotaka kuanzisha bali kurasa hujitengeneza automatically pale tu unapoandika mada mpya na kuisave, Lakini katika website ukitaka kuanzisha mada inabidi kwanza utengeneze page yake kisha ndiyo uandike mada hiyo.
  Kutokana na ugumu huo ikiwa una website na unajua kwamba utahitaji kuwa na mada nyingi za kuongeza kila muda basi ni vema ukaongeza Blog katika hiyo website ili ikurahisishie kazi hiyo.

  Mara nyingi website zinakuwa hazina taarifa nyingi sana na ndio maana nyingi zinakuwa hazina Blog ndani yake, mfano wa website ambazo hazihitaji blog ni kama vile website za vyuo, mashule, n.k kwani hakuna cha kuongeza kila siku zaidi ya kurasa maalum tu ambazo zinakuelekeza jinsi ya kujiunga na chuo fulani, uongozi wao, maabara, maktaba, ukurasa wa mawasiliano na kuhusu wao basi. Lakini website zinazokuwa na blog ni kama za habari, tuition, na mafunzo mbalimbali kwani utahitaji kila muda kuweka habari mpya au somo jipya.

  Mara nyingi website taarifa zake zinakuwa ni zilezile tu au hubadilika mara chache sana na kama kuna jambo la kuongezeka basi hutokea kwa nadra sana au kwa kipindi maalumu. Zifuatazo ni baadhi ya sifa za blog Ina sehemu ya kuacha maoni katika kila mada Inawekewa mada mpya mara kwa mara Search Engine kama vile google huitembelea mara kwa mara (Frequently crawled by Search engines) ili ijue mada mpya ulizoweka ili iweze kuziweka katika results zake pale mtu anapotafuta katika Google. Huwa na taarifa nyingi sana.

  Original from: TOFAUTI KATI YA WEBSITE NA BLOG - COMPUTER <!--if()-->- <!--endif--> - Publisher - Staryte | The Informative
   
 15. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #15
  Dec 26, 2013
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Jamiiforums na facebook zote ni social networks hakuna tofauti, tofauti iliyopo ni jf kuna majukwaa wakati facebook kuna pages. JF na FB zote ni website teknolojia iliyotumika kuziunda ndiyo tofauti.

  Nikirudi kwenye swali kuu, website na blog hazitofautiani chochote, zote ni website. Unaweza ukaruhusu comment hata hata kwenye page ya website na si katika blog tu. Blog inatakiwa iwe updated kwa habari/makala mpya na pia blog inaweza kuwa peke yake au inaweza kuwekwa ndani ya website kama unavyoona hapo juu ya jf kuna menu ya blog.

  Kwa hali ilivyo sasa ni website chache sana zinaweza kuwa bila blog ndani yake.
   
 16. Stefano Mtangoo

  Stefano Mtangoo Verified User

  #16
  Dec 26, 2013
  Joined: Oct 25, 2012
  Messages: 3,586
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  technically JF ni Discussion forums. FB ni SN... Period!

  Contradiction seem to be normal way of life... :)
   
 17. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #17
  Dec 26, 2013
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Kwenye FB hakuna discussion? SN ni nini?
   
 18. Hebie

  Hebie JF-Expert Member

  #18
  Dec 26, 2013
  Joined: Jul 29, 2012
  Messages: 1,319
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Dah! nimelipenda darasa la leo. nigefurah zaid nielimishwe namna ya kutengeza blog
   
 19. Stefano Mtangoo

  Stefano Mtangoo Verified User

  #19
  Dec 26, 2013
  Joined: Oct 25, 2012
  Messages: 3,586
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Since everything in webs is about excanging information so there is no difference btn Everything web
  Case closed!
   
 20. i

  iMind JF-Expert Member

  #20
  Dec 27, 2013
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Nafikiri kuna upotoshaji mdogo umefanyika hapa. Katika tekinolojia ya leo ya mitandao kuna vitu kama vinne hivi; websites, blog, wiki na tubes.
  website ni collection of webpages kuhusu kitu kimoja, mfano kuhusu taasisi fulani au kampuni fulani ambazo hupangwa katika mpangilio mzuri kumuwezesha msomaji kuweza kupa flow nzuri ya information.

  blog ni ukurasa mmoja ambao hueezesha mmiliki kupost mada (articles) zinaitwa blog articles. Wachangiaji wanaweza pua kutoa maoni yao na michango yao. Lakini hata kwenye website pia unaweza kuweka provision ya wasomaji kuweka maoni. Tofauti kubwa ya website na blog ni kwamba blog ni ukurasa mmoja wenye articles nyingi.

  wiki ni aina ya website kwa ajili ya kutengeneza knowledge base. Mara nyingi wiki hazihusishi maoni ila watumiaji waliojisajili wanaweza kufanya marekebisho kwenye article husika kwa lengo la kuiboresha.
  tubes ni blog maalumu kwa ajiki ya video.

  kampuni au mtu binafsi anaweza kuwa na anything.
   
Loading...