Nini tofauti ta kuula na udhamana wa cheo nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini tofauti ta kuula na udhamana wa cheo nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by tgeofrey, Jan 9, 2010.

 1. tgeofrey

  tgeofrey JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 526
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mara zote mtu ananapotata cheo hasa cha kuteuliwa tuna kauli ya ukweli tunasema kwamba fulani kaula.
  Kuula huku kuna maana gani?? Hoja hii haina maana ya kubadilishwa jinsi ya hali halisia ya jambo hili. Je kwa mawazo yako kuna uwezekano waulaji hao wakatatua matatizo ya wananchi kwa dhati ili anagalau kauli isemayo cheo ni dhamana itimie??
   
 2. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu ni kuwa kwanza hili neno 'KUULA' limeanza kama lugha ya mtaani ambayo ina tafsiri pana kidogo. Moja ya tafsiri ni 'mambo kuwa mazuri [kumnyookea] na vilevile matokeo ya ushindi katika interview, kupandishwa cheo [dhamana] , kufanikiwa inategemea mtumiaji wa neno hili ana maanisha nini kati ya tafsiri kadhaa
   
 3. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  we unafikiri zama hizi za JK utapata cheo uendelee kuwa masikini?

  1.
  zama ambazo unaruhusiwa kuwa na kampuni na ukajipa tenda ya kutoa huduma ofisini kwako?

  2.
  zama ambazo utatembea dunia nzima kwa makongamanona warsha kwa kutumia hela za wananchi

  3.
  zama ambazo ukiwa na cheo kikubwa utawapa ajira watoto wako na dugu zako wote ofisi waipendayo

  4.
  zama mabazo mtumishi wa umma anajengewa nyumba ya kuishi ya thamani ya mabilioni ya sh. na akikaribia kustaafu anakopeshwa nyumba hiyo kwa tu-milioni tuchache

  5.
  zama ambazo kufikishwa mahakamani kwa ubadhirifu inategemea umekwapua kiasi gani, kama ni kikubwa, dola yenyewe inatamka kuwa hukamatiki

  6.
  zama ambazo ukiwa mtumishi wa umma mwenye cho kikubwa unaweza kusomesha mwanao nchi yoyote uitakayo bila mawazo ya karo

  7.
  zama ambazo kutibiwa nje si kwa magonjwa ya moyo tu bali hata mafua, muhimu cheo kizuri cha khudumia umma

  8.
  nk......................nk

  sahuri yenu ambao bado mnadhani cheo ni dhamana. mimi nikimaliza shule yangu nastruggle kishenzi niwe fisadi kabla JK hajamaliza muda wake na kisha tunampigia debe aongezewe muda kwa mujibu wa katiba ili angalau ninunue ka-mgodi kwanza.

  khaaa, umasikini nimechoka mie!!!!!!!!!!
   
 4. tgeofrey

  tgeofrey JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 526
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mzee asante umenipa shule ya mwisho wa reli
   
Loading...