Nini tofauti kati ya RAM na processor?

2in1

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
211
79
Habari za mida wakuu,naomba kujuzwa tofauti za RAM na processor naona zinanichanganya.Pia ipi itakua mashine yenye uwezo mkubwa kati ya hizi mbili,machine 1:intel core i5 RAM 3GB machine2:intel core i3 RAM 4GB? Namaanisha kuwa machine 1 ina processor kubwa,RAM ndogo na machine2 ina processor ndogo,RAM kubwa
 
Kwa kifupi na lugha rahisi sana ni kuwa Ram ni eneo ambalo processor inafanyia kazi... Ukubwa wa mashine hatuangalii sana ram mkuu sababu RAM unaweza ukaongeza. what matters id processor..ukiwa na processor ndogo hata uweke 10gb ya Ram hamna kitu... ni sawa na gari pick up yenye uwezo wa tani 1 (processor)uweke bodi ya scania tani saba(RAM)..bado utaweza kubeba hiyo hiyo tani 1 tu ukizidisha gari haiendi..ila ukiwa na gari yenye uwezo wa kubeba tani saba na una bodi ya tani nne unaongeza bodi tu kwisha kazi..
 
Ni kweli RAM - Random Access Memmory ni mahari ambapo processor inaload program inapoanza kuzifanyia kazi. Kwa hiyo wakati mwingine processor inaweza kuwa nzuri kama RAM ni ndogo sana pia hutapata matokeo mazuri. Katika yote ni vema Processor ikawa kubwa ya kutosha kisha RAM.
 
Hv processor unaweza kununua kama RAM maana laptop yangu ina processor ndogo ina load muda mrefu kwenye web browser hata kufungua mafaili ina take long time
 
Kwa kifupi na lugha rahisi sana ni kuwa Ram ni eneo ambalo processor inafanyia kazi... Ukubwa wa mashine hatuangalii sana ram mkuu sababu RAM unaweza ukaongeza. what matters id processor..ukiwa na processor ndogo hata uweke 10gb ya Ram hamna kitu... ni sawa na gari pick up yenye uwezo wa tani 1 (processor)uweke bodi ya scania tani saba(RAM)..bado utaweza kubeba hiyo hiyo tani 1 tu ukizidisha gari haiendi..ila ukiwa na gari yenye uwezo wa kubeba tani saba na una bodi ya tani nne unaongeza bodi tu kwisha kazi..
Poa mkuu nimekupata fresh
 
Habari za mida wakuu,naomba kujuzwa tofauti za RAM na processor naona zinanichanganya.Pia ipi itakua mashine yenye uwezo mkubwa kati ya hizi mbili,machine 1:intel core i5 RAM 3GB machine2:intel core i3 RAM 4GB? Namaanisha kuwa machine 1 ina processor kubwa,RAM ndogo na machine2 ina processor ndogo,RAM kubwa
ni i5 ipi? ni i3 ipi? bila kuzijua aina zake ni bure, maana upo uwezekano i3 kuwa na nguvu kuliko i5 hasa kwenye laptop sababu zote ni dual core na hyperthread (ukitoa i5 quads)

pia ram inabidi uijue ni kuna ddr2, ddr3, ddr4 na kila moja inakuwa na speed zake, nyengine zinakuwa single chanell na nyengine dual chanell.
 
Iko hivi, na nadhani wengi hawajui, ila ujuzi huu utaupata kwenye nondo za zamani, speed ya processor ni combination ya processor yenyewe na front bus ya mother board, kiufundi processor ya 2 GHz ili uipate speed hiyo ni lazima clock speed za motherboard ikiwemo front bus, pci bus, na memory ziwiane, hivyo sio kila processor itafanya kazi na kila mobo, despite the interface.

RAM ni eneo amabapo data na program zinakia loaded wakati zinafanyiwa kazi, operating system yenyewe unapakiwa humo inapowasha pc yako, hizi ram pamoja na uwezo wake kwa maana ya capacity mfano 1gb,pia zina speed tofauti, na ziko ambazo ni static mwa maana hazifuti baadhi ya data ukizima mashine na ziko ambazo ni volatile zinafuta ukizima mashine hivyo kila kitu lazoma kipakiwe upya kila unapowasha.

Ni muhimu kufahamu speed ya ram kama pia inaendana na motherboard na process pia ili upate good performance.

Kuna virtual memory au virtual ram sometimes inaitwa paging, hii ni sehemu ya hard disk inayotumiwa na operating system kama ram. Kwenye window os by default hii vm hiandaliwa kwa kuchukua kiasi cha physical ram iliyopachikwa kwenye motherboard zidisha kwa 1.5 mfano kama ram ni 1gb zidisha 1.5 utapata hiyo vm ni 1.5g lakini unaweza ongeza manually.

Kwa ujumla kasi ya compyuta inategemea vitu vingi sana, kabla processor haijachungulia kwenye ram ili ianze kuchakata mambo kwanza inangaalia level 1 cache, hii huwa ndogo na hiwa karibu na processor na siku hizi wanaijumuisha kwenye processor yenyewe kabisa, kula level2 cache, na kama iko level 3 nayo itaaangaliwa then ndio unakwenda kwenye ram, then inakwenda kwenye hard disk,

Vyote hivi vinapaswa kuwa katika ubora fulani, so unaweza kuwa na ptocessor nzuri tu na ram ya kutosha lakini hard drive ikawa slow na uk experience slowness..

Kuna mengi ya kujifunza hapa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom