Nini tafasiri halisi ya neno 'wanyonge' Tanzania yetu hii?

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
1,346
1,303
Imezoeleka sasa kwa viongozi wengi kutuita wanyonge. Lakini kwa nini watumie neno hili?

Kwangu napata majibu yafuatayo:

1. Unyonge ni hali ya mtu kushindwa kujitetea hata kama anaporwa haki zake. Kibinadamu kuna vitu vya msingi ili maisha yaendelee. Elimu, afya bora, makazi salama na kumudu kuhudumia familia kupata mlo bora.

2. Unyonge ni pale mtu uunaposhindwa kuchagua na kuchaguliwa kutimiza hali yako ya kidemokrasia. Ukiwa mnyonge huwezi kuchaguliwa na hata ukitaka kuchagua huwezi kutimiza matakwa yako utapewa kofia, khanga na t shirt ili ubadili maamuzi.

3. Ukiwa mnyonge wale walio na dola watafanya kila namna wakutishe ili ubaki ukiwa mtumwa wa mawaxo na fikra. Sasa tafadhali tusiitane tena wanyonge.

This time wanyonge tunamhuhitaji rais mnyonge. Aliyetishwa, kuteswa, kudhulumiwa na sasa yuko nasi.

Karibu Tundu Lissu, hii ndiyo sifa tulkyokupa. Hao wengine waendelee na maflyover zao huku village tunahitaji maji, vifaa vya kutosha mashuleni na hospitali na barabara za kupitika misimu yote.
 
But remember you did it already in the past five years
I never thought it could be in this way. I placed my vote to person think he would be full of good governance and leadership as well as transparent yet he turned to be a ruler instead.
I wont cast my vote to him to him
 
Kwa ufupi wanyonge ni malofa, watu wasiojitambua, waliochapika kwa umaskini uliotukuka, hawana hili wala lile.. (mtazamo wangu) matumizi ya neno hili ni kejeli kwa watanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom