Nini solution ya matiti yasiyo ya kawaida kwa mwanaume?

future mind

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
221
229
Naombeni msaada wenu wanajamii hili tatizo ya gynecomastia nimekuwa likiniumiza kichwa kwa muda mrefu sana bila ya mafanikio, nakosa raha kabisa. yaani nimekuwa discomfort kiasi cha kukosa hata confidence mbele za watu. Naombeni msaada wenu nifanye nini niweze kuwa katika hali ya kawaida.

1582120096480.png
 
Nenda gym mkuu tandika tizi la hatari yenyewe yatasepa ayo itabaki kuwa kifua
 
Pole Mkuu, kama walivyoelezea waliotangulia suluhisho la tatizo lako litategemeana na chanzo cha tatizo lako. Ni kweli huu ugonjwa una-embarrassy na kupunguza confidency lakini kwa kiasi kukubwa sio hatarishi. Kabla hujaenda kumwona Daktari wako kwa uchunguzi wa kina sio vibaya tukijadili kwa juujuu baadhi ya vitu vinavyosababisha hili tatizo.

=Kwanza kabisa hali hii inatokana na uwiano usio sahihi wa Hormones za ESTROGEN na TESTOSTERONE (hormone ya Testosterone inakuwa chini zaidi kulinganisha na Estrogen)
=Hali hii inaweza kuwa ya kawaida kwa watoto wachanga,wavulana wanaobalehe na wazee.
Mambo mengine yanayoweza kuleta mushkeli kwenye balance ya hizo homone kwa uchache ni:
-Dawa mbalimbali za binadamu kama baadhi ARVs n.k,n.k
-Pombe na mihadarati
-Baadhi ya dawa za miti shamba
-Magonjwa balimbali kama= Kusinyaa kwa kokwa (Hypogonadism) -usijali tafsiri sio fasaha
Uvimbe kwenye kokwa, adrenal glands, ubongo(pituitary)

=,matatizo ya tezi la thyroid (hyperthyroidism)
=matatizo ya figo(kidney failure)
=matizo ya Ini hasa ugonjwa wa Cirrhosis
=Vilevile Lishe duni na njaa kali ya muda mrefu(starvation) vinaweza kusababisha.

Kwa hiyo, suluhisho litategemeana na chanzo, ila kama ni uzee hamna namna labda operation ya kuondoa breast tissue. Kama sababu ni dawa zinabadilishwa. Tusubiri wataalamu waje tutapata ufafanuzi zaidi maana kwa kuangalia ID lazima tunao wengi tuu humu.
 
damian marijani,
Asante sana mkuu kwa ufafanuzi wako, ila ili tatizo nimejaribu kulifwatilia hata nimemuuliza doctor mmoja ninaemfahamu akaniambia si jambo ya kushtuka ni kitu cha kawaida.

Ila kwa Mimi nimeshindwa kabisa kulichukulia kwamba nijambo ya kawaida kwani najikuta nipo tofauti na wengine afu pia nimejaribu kufwatilia kwenye google nimeona kuna dawa ya kupunguza inaitwa gynexin Ila sasa hii dawa cijui naipataje na je ni kweli ndo solution ya tatizo hili?

Kama kuna MTU anaifahamu hii dawa " gynexin " naomba atueleze
 
Mkuu tafuta 2nd opinion kwa daktari mwingine, sisitiza akufanyie uchunguzi wa kina kuhakikisha kuwa tatizo lako chanzo chake sio katika hayo tuliyotaja.

Baada ya hapo unaweza ujipe kama miaka miwili hivi ukijiangalia kwani tatizo linaweza kuisha lenyewe. Kama tatizo linaendelea unaweza kujaribu dawa na baadaye hata operation ikishindikana.
 
Mkuu tafuta 2nd opinion kwa daktari mwingine, sisitiza akufanyie uchunguzi wa kina kuhakikisha kuwa tatizo lako chanzo chake sio katika hayo tuliyotaja. Baada ya hapo unaweza ujipe kama miaka miwili hivi ukijiangalia kwani tatizo linaweza kuisha lenyewe. Kama tatizo linaendelea unaweza kujaribu dawa na baadaye hata operation ikishindikana.
Poa mkuu asante sana kwa ushauri wako
 
Back
Top Bottom